DARASA LA SABA WAONDOLEWA KATIKA AJIRA ZA JWTZ

 


SERIKALI Imeondoa Utaratibu Wa Kuandikisha Ajira Kwa Vijana Wanaohitimu Elimu Ya Darasa La Saba Kwenye Jeshi La Wananchi Tanzania (JWTZ).

Hayo Yamesemwa Leo Mei 20,2024 Na Naibu Wa Ardhi, Nyumba Na Maendeleo Ya Makazi, Godfrey Pinda Kwa Niaba Ya Waziri Wa Ulinzi Na Jeshi La Kujenga Taifa, Alipokuwa Akijibu Swali La Mbunge Wa Ushetu, Emmanuel Cherehani.

Cherehani Amehoji Kuna Mpango Gani Wa Kuongeza Nafasi Za Ajira Na Mafunzo Jeshini Kwa Vijana Wanaomaliza Darasa La Saba Na Kidato Cha Nne.

Akijibu Swali Hilo, Pinda Amesema JWTZ Huandikisha Askari Wapya Kwa Mujibu Wa Sheria, Kanuni Na Maelekezo Yanayotolewa Mara Kwa Mara.

Amesema Utaratibu Wa Kuandikisha Askari Wapya Umefafanuliwa Kwenye Kanuni Ya 5 Ya Kanuni Za Majeshi Ya Ulinzi Juzuu Ya Kwanza (Utawala).

“Serikali Imeaondoa Utaratibu Wa Kuandikisha Ajira Kwa Vijana Wanaohitimu Elimu Ya Darasa La Saba,”Amesema.

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT