VYOMBO vya habari vya serikali vinasema Rais Ebrahim Raisi alikuwa kwenye helikopta ambayo ilitua kwa shida siku ya Jumapili.
Pia ilisemekana kumbeba
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian.Waziri wa Mambo ya Ndani
alisema waokoaji bado wanajaribu kufika eneo hilo kutokana na hali ngumu ya
hewa.Hali ya waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo bado haijajulikana kwa sasa,
huku ripoti kuwa bado hakuna mawasiliano yaliyofanywa.
Kwa mujibu wa vyombo vya
habari vya ndani, Rais Raisi alikuwa akielekea katika mji wa Tabriz, kaskazini
magharibi mwa Iran, baada ya kurejea mpakani na Azerbaijan, ambako alifungua
mabwawa ya Qiz Qalasi na Khodaafarin.
Ukungu mkubwa unafanya
msako kuwa mgumu katika eneo ambalo inadhaniwa kuwa huenda helikopta hiyo
ilitua, kulingana na ripota wa shirika la habari la Fars.
Alisema mwonekano katika
eneo la milima na misitu ulikuwa chini hadi takriban mita tano tu.Eneo hilo ni
kama kilomita 50 kaskazini mwa Tabriz.
Ahmad Alirezabeigi,
Mbunge wa Iran katika mji wa Tabriz amewaambia waandishi wa habari mjini Tehran
kwamba waokoaji bado hawajapata eneo la helikopta iliyombeba rais na waziri wa
mambo ya nje.
Aliongeza kuwa helikopta
nyingine mbili katika msafara huo zilitua salama.Kanda za video zimeibuka
kwenye televisheni ya taifa zikionyesha waumini wakimuombea afya rais katika
mji mtakatifu wa Mashhad.
Rais wa Iran Ebrahim
Raisi ni nani?
Bw Raisi, 63,
alichaguliwa kuwa rais katika jaribio lake la pili mwaka wa 2021.
Anaonekana kama mhubiri
mwenye msimamo mkali na anachukuliwa kuwa mrithi wa Ayatollah Khamenei siku
moja, kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu 1989.
Mnamo mwaka wa 2019,
Kiongozi Mkuu alimteua kwenye nafasi yenye nguvu ya mkuu wa mahakama.
Bw Raisi pia alichaguliwa
kuwa naibu mwenyekiti wa Bunge la Wataalamu, baraza la makasisi lenye wanachama
88 walio na jukumu la kumchagua Kiongozi Mkuu ajaye.