RASMI Sasa Miamba Miwili
Ya Soka Nchini Yanga Na Azam Fc Zitakutana Katika Fainali Ya Kombe La Crdb
(Cbfc), Ambayo Inatarajiwa Kuchezwa Juni 2, Mwaka Huu Kwenye Uwanja Wa
Tanzanite, Uliopo Mjini Babati Mkoani Manyara.
Azam Ilifuzu Hatua Hiyo
Baada Ya Ushindi Mnono Wa Mabao 3-0, Dhidi Ya Coastal Union Yaliyofungwa Na
Nyota Wa Kikosi Hicho, Abdul Suleiman 'Sopu' Aliyefunga Mawili Na Feisal Salum
'Fei Toto', Mechi Ikipigwa Uwanja Wa Ccm Kirumba Mwanza.
Huku Yanga Yenyewe
Ikifika Hapa Baada Ya Kuibuka Na Ushindi Wa Bao 1-0 Dhidi Ya Ihefu Kwenye
Mchezo Mkali Uliopigwa Kwa Dakika 120 Kwenye Uwanja Wa Sheikh Amri Abeid Mkoani
Arusha.
Hii Ni Fainali Ya Nne Kwa
Azam Fc Katika Mashindano Haya Ambapo Mara Tatu Ilizotinga Imelichukua Mara
Moja Tu Ikifanya Hivyo Msimu Wa 2018-2019, Ilipoifunga Lipuli Ya Mkoani Iringa
Bao 1-0, Mechi Iliyopigwa Kwenye Uwanja Wa Ilulu Lindi.
Mchezo Huo Uliopigwa Juni
Mosi, 2019, Bao Pekee La Azam Lilifungwa Na Aliyekuwa Mshambuliaji Wa Timu Hiyo
Mzambia, Obrey Chirwa Dakika Ya 64.