MTANDAO Wa Youtube
Umetangaza Kuanzisha Vikwazo Kwa Video Zinazohusisha Bunduki Baada Ya
Malalamiko Mengi Kutoka Kwa Wanaharakati.
Kwa Muda Mrefu Sasa Wanaharakati Wamekuwa Wakiukosoa Mtandao Huo Kwa Kuweka
Wazi Maudhui Yanayotia Kiwewe Na Kuhamasisha Vurugu.
Utafiti Uliyofanywa Na Taasisi Moja Ya Masuala Ya Afya Umebaini Kuwa Tokea
Mwaka 2020 Majeraha Yatokanayo Na Bunduki Ndio Sababu Inayoongoza Kupelekea
Vifo Vya Watoto Na Vijana Nchini Marekani.
Kuanzia Juni 18, Mtandao Huo Unaomilikiwa Na Kampuni Ya Google Utazuia Video
Yoyote Inayoonyesha Namna Ya Kuondoa Vifaa Vya Usalama Wa Bunduki.
Vilevile Mtandao Huo Utazuia Video Zinazoonyesha Bunduki Za Kutengeneza
Majumbani Na Silaha Za Kiotomatiki Kwa Watumiaji Walio Chini Ya Umri Wa Miaka
18.
Tags
INTERNATIONAL