SHIRIKA La Huduma Ya
Wanyamapori Nchini Kenya Kws Limetangaza Utekelezaji Wa Mpango Wa Kuwaua
Kunguru Hao Kabla Ya Tarehe 31 Disemba 2024.
Mkurugenzi Wa Wanyamapori
Na Huduma Za Jamii Profesa Charles Musyoki, Ameeleza Kuwa Mpango Huo Wa
Kuwaondoa Kunguru Wa Nyumbani Ni Kwa Ajili Kulinda Afya Za Watu Dhidi Ya Ndege
Hao Wakubwa Weusi Na Kuongeza Kuwa Serikali Itashughulikia Tatizo Hilo.
Ndege Hao Wametajwa
Kusababisha Uvamizi Na Usumbufu Mkubwa Kwa Wakazi Na Sekta Ya Utalii Haswa
Biashara Ya Hoteli Maeno Ya Pwani Ya Mombasa, Malindi, Watamu Na Kilifi.
Kunguru Ni Ndege Wa
Kawaida Wa Familia Ya Kunguru (Corvidae) Wajulikanao Kama Kunguru Wa Nyumbani
(Corvus Splendens) Wenye Asili Ya Bara Asia.
Hata Hivyo, Kwa Sasa
Hupatikana Katika Sehemu Nyingi Ulimwenguni, Baada Ya Kufika Kwa Njia Ya Meli.
Kunguru Walifika Nchini
Kenya Mnamo 1947 Huku Idadi Yako Ikizidi Kuongezeka Tangu Wakati Huo Na Kuwa
Kero Kubwa Katika Maeneo Ya Pwani.
Kunguru Hao Pia Wametajwa
Kuleta Usumbufu Kwa Kwa Watu Katika Mataifa Ya Tanzania, Sudan, Somalia, Misri,
Msumbiji, Djibouti Na Ethiopia.