MKUU WA MAJESHI Ya Ulinzi
Jenerali Jacob John Mkunda Amewavisha Nishani Maafisa Na Askari Wa Vikosi Vilivyoko
Kanda Ya Dar Es Salaam Na Pwani Kwa Niaba Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan.
Zoezi Hilo Limefanyika Jijini
Dar Es Salaam Kwenye Uwanja Wa Mgulani Tarehe 7 Juni 2024 Kwa Kuwavisha Nishani
Ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, Nishani Ya Utumishi Mrefu Na Nishani Ya Utumishi
Mrefu Na Tabia Njema.
Wakati Huo Huo, Jenerali
Mkunda Amewavisha Nishani Ya Ulinzi Wa Amani Ya SADC Maafisa Na Askari Kwa
Niaba Ya Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC Kwa Kutambua Mchango Wao
Katika Ulinzi Wa Amani Nchini Msumbiji Chini Ya Mwavuli Wa SADC Iliyowatunuku Nishani
Hiyo.