MAHAKAMA
KUU Masjala Ndogo Ya Iringa Imemuachilia Huru Dotto Kisinga, Aliyekuwa
Akitumikia Adhabu Ya Kifungo Cha Maisha Jela Kwa Kosa La Kumwingilia Kingono
Binti Yake Mwenye Umri Wa Miaka Sita, Baada Ya Kubatilisha Hukumu Iliyomtia
Hatiani.
Dotto
Alihukumiwa Adhabu Hiyo Na Mahakama Ya Wilaya Iringa Baada Ya Kumtia Hatiani
Kwa Kosa La Kujamiiana Kinyume Na Kifungu Cha 158 (L) (A) Na 161 Vya Sheria Ya Kanuni
Ya Adhabu.
Kwa
Mujibu Wa Hati Ya Mashtaka, Alitenda Kosa Hilo Aprili 15, 2023, Wakati Mama Wa
Mwathirika Alipokwenda Mashine Kusaga Unga Na Ndugu Zake Wa Kiume Walipokuwa
Wamekwenda Kucheza.
Hata
Hivyo, Mahakama Kuu Katika Hukumu Yake Iliyotolewa Na Jaji Ilvin Mugeta, Jumanne
Juni 11, 2024, Kufuatia Rufaa Aliyoikata Dotto, Imemuondolea Hatia Hiyo Baada
Ya Kutilia Shaka Ushahidi Wa Upande Wa Mashtaka Hasa Wa Mtoto Mwathirika.
Kwa
Mujibu Wa Ushahidi Katika Kumbukumbu Za Mahakama, Mtoto Huyo Anaishi Na Wazazi
Wake Na Ndugu Zake Wengine Wawili Wa Kiume.
Mtoto
Huyo Aliibua Taarifa Za Kuingiliwa Na Baba Yake Aprili 17, 2023, Mbele Ya Ofisa
Ustawi Wa Jamii Wa Halmashari Ya Wilaya Iringa Anayeshughulikia Dawati La Wenye
Uhitaji Maalumu Wakiwamo Watoto, Gladness Amulike Ambaye Ni Shahidi Wa Kwanza
Upande Wa Mashtaka (SMI).
Siku
Hiyo, Amulike Alifika Shule Ya Msingi Ulata Kutoa Elimu Kuhusu Usalama Wa
Watoto Na Unyanyasaji Wa Kijinsia, Akiwa Na Askari Polisi G.3553, CPL Salum, (SM3)
Katika Kesi Hiyo.
Baada
Ya Kutoa Elimu Hiyo, Ndipo Mtoto Huyo (SM2) Alijitokeza Na Kueleza Kuwa Baba
Yake Humwingilia Kingono Na Ameshafanya Hivyo Mara Sita Na Kwamba Wakati
Mwingine Hufanya Hivyo Mchana Watu Wanapokuwa Hawapo Nyumbani.
Alidai
Kuwa, Mwaka 2022 Alimuingilia Mara Tatu Na Alimtishia Asiseme Chochote.
Hata
Hivyo, Alimfahamisha Mama Yake Juu Ya Tukio Hilo Lakini Hakuchukua Hatua Ingawa
Kutokana Na Athari Hizo Za Kuingiliwa Alikuwa Akimtibu Majeraha Ya Kutoka Damu
Sehemu Yake Ya Siri.
Amulike
Baada Ya Kuwahoji Watoto Wawili Wa Kiume Na Wao Walikiri Kulawitiwa.
Mtoto
Huyo Alifanyiwa Uchunguzi Na Daktari Kelvin Prosper Maro Ambaye Alibainisha
Kuwa, Alikuwa Na Dalili Za Kuingiliwa Kwa Vile Sehemu Yake Ya Siri Ilikuwa Wazi
Na Bikra Haikuwepo, Lakini Hakuona Michubuko.
Hivyo,
Mtuhumiwa Alitiwa Mbaroni Na Kisha Akapandishwa Kizimbani Na Kusomewa Shtaka
Hilo.
Mbali
Na Mshtakiwa Katika Ushahidi Wake Kupinga Ushahidi Wote Wa Upande Wa Mashtaka,
Mama Wa Mtoto Huyo Ambaye Ni Shahidi Wa Pili Wa Utetezi (SU2) Alikana Kuambiwa
Na Mtoto Wao Kuingiliwa Na Babake Wala Kumtibu Kwa Dawa Za Kienyeji.
Mahakama
Ya Wilaya Ilipuuza Ushahidi Huo Akieleza Kuwa, Utetezi Haukutikisa Ushahidi Wa
Mashtaka Badala Yake Iliridhika Na Ushahidi Wa Upande Wa Mashtaka Na Ikamtia
Hatiani Na Kumhukumu Kutumikia Adhabu Hiyo Ya Kifungo Cha Maisha Jela.
Rufaa
Na Hoja Zilizotolewa
Hata
Hivyo, Dotto Alikata Rufaa Akipinga Hukumu Yote Yaani Hatia Na Adhabu, Huku
Akitoa Sababu Tisa Za Rufaa Ambazo Hoja Ya Msingi Alidai Kuwa Mashtaka Dhidi
Yake Hayakuthibitishwa Bila Kuacha Shaka Ya Msingi.
Siku
Ya Kusikiliza Rufaa Hiyo, Mrufani, Dotto Alieleza Kwamba Hajui Kusoma Wala
Kuandika, Hivyo Aliomba Maelezo Yake Ya Maandishi Aliyoandaliwa Na Wenzake
Gerezani Yapokewe Na Mahakama Iyatumie Kama Hoja Zake Kuunga Mkono Sababu Zake
Za Rufani.
Hoja
Yake Kubwa Ilikuwa Kwamba Hakuna Ushahidi Kuwa Tukio Lilitendeka Aprili 15,
2023 Kama Inavyodaiwa Kwenye Hati Ya Mashtaka.
Wakili
Wa Serikali, Winfrida Mpiwa Alieleza Kuwa Jamhuri Inaunga Mkono Rufaa Hiyo Kwa
Kuwa Shtaka Halikuthibitika Kwa Kuwa Katika Ushahidi Wake, Mtoto Mwathirika
Hakueleza Tarehe Ya Tukio, Bali Tarehe Ya Tukio Ilitajwa Na Shahidi Mpelelezi
Ambaye Ushahidi Wake Ni Wa Kuambiwa.
Alieleza
Kuwa, Pale Ambako Tarehe Na Muda Wa Tukio Vimetajwa Katika Hati Ya Mashtaka,
Lazima Vithibitishwe Katika Ushahidi Na Kwamba Katika Kesi Hiyo, Ushahidi Huo
Haupo.
Uamuzi Wa Mahakama Kuu
Jaji
Mugeta Amekubaliana Na Hoja Ya Mrufani Kwamba Tarehe Ya Tukio Iliyotajwa Kwenye
Hati Ya Mashtaka Haikuthibitishwa Na Kwamba Kutothibitisha Tarehe Ya Tukio
Maana Yake Shtaka Halikuthibitishwa.
Amesema
Shahidi Wa Kwanza Na Wa Tatu Wa Upande Wa Mashtaka Walijaribu Kueleza Tukio
Lilivyotendeka, Lakini Akasema Ushahidi Wao Ni Wa Kuambiwa Na Mwathirika Au
Ndugu Zake Wa Kiume Ambao Hata Hivyo Hawakuletwa Mahakamani Kutoa Ushahidi.
Jaji
Mugeta Amesema Kinachosikitisha Maelezo Mazuri Ya Mashahidi Hao Kuhusu Tukio
Lilivyotendeka, Muda Na Mahali, Hayako Katika Ushahidi Wa Mwathirika.
“Kama
Mwathirika (SM2) Aliweza Kuyasema Haya Yote Kwa SM3 (Mpelelezi) Na Mengine
Mengi Kwa SMI (Ofisa Ustawi Wa Jamii), Inasikitisha Kwamba Hakuyasema
Mahakamani. Habari Za Muda Wa Tukio, Usiku Au Mchana, Kutishiwa Na Kutibiwa Na
Mama Yake Kwa Dawa Za Kienyeji Hazipo,” Amesma Jaji Mugeta.
Hivyo,
Amesema Ushahidi Wa Mashahidi Hao Kuhusu Tukio Kwa Kuwa Ni Wa Kuambiwa,
Haukubaliki Chini Ya Kifungu Cha 62 Cha Sheria Ya Ushahidi.
Jaji
Mugeta Amesema Hakimu Aliyesikiliza Kesi Hiyo Alipuuza Ushahidi Wa Mama
Wa Mwathirika Huyo Aliyekana Kuambiwa Taarifa Za Mtoto Huyo Kuingiliwa Wala
Kumtibia Kwa Dawa Za Kienyeji, Bila Hata Kueleza Ni Ushahidi Upi Wa Utetezi Na
Kwa Nini Anaona Ushahidi Wa Mashtaka Haujatikiswa.
Hivyo,
Jaji Mugeta Amesema Anakubaliana Na Hoja Ya Mrufani Kuwa Utetezi Wa
Mrufani Haukuzingatiwa Kwa Sababu Hukumu Inayolalamikiwa Haina Uchambuzi Wa
Kina Wa Utetezi.
Amesema
Hakimu Angezingatia Ushahidi Wa Utetezi Angeona Kwamba Ushahidi Alioutumia
Kumtia Hatiani Mrufani Ulikuwa Ni Wa Kuambiwa Na Ulikanushwa Barabara Na
Utetezi Wa Mrufani.
“Katika
Utetezi Wake Mrufani Alisema Kama Mwathirika Angekuwa Ameingiliwa Kinguvu, Uke
Wake Ungechanika Na Asingeweza Kutembea Sawasawa Kwa Kuzingatia Umri Wake,”
Amesema Jaji Mugeta.
“Ninakubaliana
Na Hoja Hii. Mtoto Wa Miaka Sita Hawezi Kuingiliwa Kingono Na Mtu Mzima
Akabakia Salama. Katika Ushahidi Wake Daktari (SM4) Alisema Uke Haukuwa Na
Michubuko.”
Jaji
Mugeta Amesema Kuwa, Ameshindwa Kumwamini Mtoto Huyo Kuwa Aliingiliwa Na Baba
Yake Na Asimweleze Mama Yake Na Kwamba Kitendo Cha Mama Yake Kusimama Dhidi
Yake Kinaashiria Kuwa Mtoto Huyo Alisema Uongo.
“Kwa
Umri Wake Na Kwa Kuzingatia Mazingira Ambayo Tuhuma Iligunduliwa, Ushahidi Wake
Unapaswa Kuchukuliwa Kwa Tahadhari. Rufaa Hii Ina Mashiko, Imeshinda. Mahakama Ya
Chini Ilipotoka Katika Kuchambua Ushahidi Na Kumpata Mrufani Na Hatia,” Amesema
Jaji Mugeta Na Kuhitimisha:
“Kwa
Sababu Hiyo Hatia Hiyo Nimeifuta Na Adhabu Yake Nimeibatilisha. Mrufani Aachiliwe
Huru Mara Moja Isipokuwa Kama Kuna Sababu Nyingine, Tofauti Na Amri Ya Kesi
Hii, Ya Kuendelea Kumshikilia Gerezani.”
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI