RAIS Dkt. Samia Suluhu
Hassan amekabidhiwa tuzo maalumu kwa kutambuliwa mchango wake katika
kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, tuzo ambayo imetolewa na
wabunge wanawake kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi Kupikia Duniani
Akizungumza Hapo Jana Juni 7,2024 katika maadhimisho hayo Spika wa Bunge Dk.Tulia
Ackson aliyekuwa mgeni rasmi amesema kuna kila sababu za Rais Dk.Samia kupewa
tuzo na wabunge hao pamoja na Oryx kwani amekuwa kinara katika nishati safi ya
kupikia na juhudi zake zinashuhudiwa na Watanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.
Amesema Rais Samia alipokuwa Dubai na hivi karibuni alipoenda katika mkutano
uliofanyika Paris ametambulika na dunia nzima kama kinara wa nishati safi ya
kupikia.Hivyo wanaendelea kusisitiza Rais Samia ndiye kinara wa nishati safi ya
kupikia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema katika
kutambua mchango wa Rais Samia katika nishati safi wameamua kutoa tuzo kwa Rais
kama sehemu ya kumuunga mkono kwa juhudi anazofanya kuhamasisha matumizi ya
nishati hiyo.