RAIS WA KENYA William Ruto Amesema Kuwa Nchi
Yake Inaunga Mkono Wito Wa Papa Francis, Wa Kusitishwa Mapigano Na Kupatikana
Amani Ya Kudumu Nchini DRC Na Sudan.
Rais
Ruto Aliyasema Haya Baada Ya Kikao Cha Faragha Na Kiongozi Huyo Wa Kanisa Katoliki,
Wakati Wa Mkutano Wa Nchi 7 Tajiri Duniani (G7) Uliofanyika Mjini Apulia, Italia.
''Tuna
Imani Kwamba Makundi Yanayopigana Yatakubali Kusitisha Mapigano Na Kutoa Nafasi
Ya Amani,'' Alisema Rais Ruto Katika Taarifa Fupi Katika Mtandao Wa X.
Katika
Fursa Nadra Ya Kuhutubia Mkutano Huo Wa G7, Rais Ruto Alisisitiza Haja Ya Jamii
Ya Kimataifa Kuwajibikia Suala La Upatanishi Kuondoa Migogoro Ya Duniani.
''Ninatoa
Wito Kwa Viongozi Wa Dunia Kuhamasishwa Kuchukua Hatua Kabambe Ya Pamoja Ili
Kukabiliana Na Matatizo Ya Kimataifa,'' Alisema Rais Ruto.
AU
- Wakala Wa Amani
Rais
Ruto Pia Aliweka Wazi Mipango Wa Mataifa Ya Afrika Ya Kufanya Marekebisho Ya
Kimkakati Na Dhamira Ili Kuweza Kukabiliana Na Majanga, Ikiwemo Migogoro Ya
Ndani.
''Afrika
Imedhamiria Kutekeleza Sehemu Yake Kikamilifu, Na Ndiyo Maana AU Imewekewa
Mageuzi Makubwa Ya Kimkakati Ili Kuwa Wakala Muhimu, Unaotambuliwa Na
Kushughulikiwa Na Jumuiya Ya Kimataifa Ili Kushughulikia Changamoto Zetu Za
Pamoja Na Kukuza Ustawi Wetu Wa Pamoja,'' Alisema Rais Ruto.
Ajenda
Kuu Ya Mkutano Huo Ulikuwa Uhamiaji, Akili Mnemba Na Usalama Wa Kiuchumi,
Viongozi Wa G7 Walisisitiza Azma Yao Ya Kukabiliana Na Changamoto Za Kimataifa
"Katika Wakati Muhimu Katika Historia."
Hata
Hivyo Msaada Wa Kifedha Kwa Ukraine, Vita Vya Gaza, Mabadiliko Ya Hali Ya Hewa,
Iran, Hali Ya Bahari Ya Shamu, Usawa Wa Kijinsia Na Sera Ya Viwanda Na Usalama
Wa Kiuchumi Wa China Vilionekana Kutawala Mkutano.
Mgawanyiko
Uliibuka Wakati Wa Mkutano Huo, Hata Hivyo, Haswa Juu Ya Kukosekana Kwa Marejeleo
Ya Uavyaji Mimba Katika Tamko La Mwisho La Mkutano Huo.
Lakini
Alipoulizwa Na Waandishi Iwapo Kuna Muafaka Juu Ya Migogoro Mikubwa Duniani, Rais
Wa Ufaransa Emmanuel Macron Alikemea Kuwa Hilo Halikuwa Sababu Yamkutanu Huo.
"Lengo
La G7 Ni Kuunda Muunganiko Na Kuweza Kuondoa Kutokuelewana. Sio Mahali Ambapo
Unaamua Hatua Za Dharura Au Kudhibiti Mambo," Alisema Macron.
Mbali
Na Mataifa Ya G7 Ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza Na Marekani,
Wenyeji Wa Italia Pia Waliwaalika Viongozi Kadhaa Wa Afrika - Rais Wa Algeria
Abdelmadjid Tebboune, Rais Wa Kenya William Ruto Na Rais Wa Tunisia Kais Saied.
Lakini
Mashirika Ya Kutetea Haki Za Binadamu Yalikashifu Kile Walichokisema Ni Ukosefu
Wa Ari Ya Kuunga Mkono Nchi Zinazoendelea.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI