MWENYEKITI
Wa Chadema Kanda Ya Nyasa, Joseph Mbilinyi Maarufu Kwa Jina La Sugu, Ameshauri
Namna Ya Kuunasua Mchakato Wa Katiba, Akitaka Rasimu Ya Katiba Iliyoandaliwa Na
Tume Ya Jaji Joseph Warioba Irejeshwe Ili Ipigiwe Kura Na Wananchi.
Sugu
Amesema Hatua Hiyo Itasaidia Kuokoa Mabilioni Ya Fedha Yaliyotumika Katika
Mchakato Wa Mabadiliko Ya Katiba Ambayo Haikupatikana.
Mchakato
Huo Ulianzishwa Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne, Jakaya Kikwete Mwaka 2012
Alipounda Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba Ambayo Ilikusanya Maoni Ya Wananchi Na
Kuandika Rasimu Ya Katiba.
Rasimu
Hiyo Ilipelekwa Katika Bunge Maalum La Katiba Na Kujadiliwa, Lakini Baadhi Ya
Vyama Vya Upinzani Vilisusia Bunge Hilo Na Kujitoa. Kwa Upande Wa Vyama Na
Wadau Wengine Waliobaki Ikiwemo CCM Walitoka Na Rasimu Ya Katiba Inayopendekezwa.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI