VIONGOZI Mbalimbali Wa Ulaya,
Wamelaani Vikali Shambulio Dhidi Ya Waziri Mkuu Wa Denmark Mette Frederiksen
Mwanasiasa Huyo
Alishambuliwa Katika Viwanja Vya Mjini Copenhagen Jana Ijumaa, Na Kuzidisha
Wasiwasi Wa Ongezeko La Ghasia Barani Ulaya.
Waziri Mkuu Frederiksen,
Mwenye Umri Wa Miaka 46, Alishambuliwa Ijumaa Jioni Kwa Kupigwa Katika Viwanja
Vya Kultorvet Na Ameeleza Kushutushwa Na Tukio Hilo. Ofisi Yake Hata Hivyo
Haikutoa Maelezo Zaidi Ikiwa Kiongozi Huyo Alijeruhiwa.
Mashuhuda Waliozungumza
Na Vyombo Vya Habari Vya Denmark, Wameeleza Kuwa Waziri Huyo Mkuu Aliweza
Kuondoka Kwa Kutembea Kutoka Eneo La Tukio.
Polisi Tayari Wanamshikilia
Mwanaume Mwenye Umri Wa Miaka 39 Anayeshukiwa Kuhusika Na Shambulio Hilo, Na
Amefikishwa Katika Mahakama Mjini Copenhagen Leo Jumamosi.