NAIBU Waziri
Wa Madini Dkt. Steven Kiruswa Amewataka Vijana Nchini Kuchangamkia Fursa
Zilizopo Katika Sekta Mbalimbali Ikiwepo Ya Madini Kama Ajira Mbadala Na Namna
Ya Kujikwamua Kiuchumi Wao Binafsi Na Familia Zao Sambamba Na Kuongeza Mchango
Wao Katika Maendeleo Ya Taifa Kwa Ujumla.
Amesema Hayo Mei 17, 2024
Wilayani Longido Mkoani Arusha Wakati Akizungumza Katika Kongamano La Vijana Wilayani
Humo, Ambalo Limelenga Kuwasaidia Vijana Kufahamu Fursa Zilizopo Katika Sekta
Za Madini, Kilimo, Ufugaji Pamoja Na Mikopo Ya Halmashauri Kwa Vikundi Ya Wanawake,
Vijana Na Walemavu.
Dkt. Kiruswa Amesema,
Kutokana Na Changamoto Zilizopo Katika Soko La Ajira Hivi Sasa Ulimwenguni
Kote, Ni Wakati Wa Vijana Kuhamisha Fikra Na Nguvu Zao Katika Ajira Mbadala Na
Kwamba Fursa Zilizopo Katika Sekta Mbalimbali Kama Vile Programu Ya Mining For
A Brighter Tomorrow (MBT) Pamoja Na Sekta Binafsi Zinatoa Nafasi Kwa Vijana
Wenye Elimu Na Waliyokosa Fursa Za Kusoma Kufikia Vyuo Vya Kati Na Vyuo Vikuu.
“Mataminio Ya Mheshimiwa
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ni Kuona Vijana Wanachamgamkia Fursa Za Ajira
Mbadala Ili Kunufaika Na Fursa Mbalimbali Zilizopo Katika Sekta Binafsi Na
Ametuelekeza Kuwasadia Vijana Kufahamu Fursa Hizo Na Kuwawezesha Kimbinu Pamoja
Na Mitaji Kufikia Ndoto Zao,” Amesema Dkt. Kiruswa.
Aidha, Dkt. Kiruswa Amewataka
Vijana Kuunda Vikundi Ili Wanufaike Na Mikopo Ya Asilimia 10 Ya Halmashauri Kwa
Ajili Ya Vikundi Vya Wanawake, Vijana Na Walemavu Ili Kujikwamua Kiuchumi Kwa
Kuwa Serikali Imeshafanyia Marekebisho Namna Ya Usimamizi Wa Mikopo Hiyo Na
Mwaka Ujao Wa Fedha Itaanza Kutolewa Kwa Vikundi Hivyo.
Kwa Upande Wake, Mkuu Wa Wilaya
Ya Longido,Mhe. Marko Ng’umbi Amewataka Vijana Kuzingatia Mafunzo Na Maarifa
Waliyoyapata Kwenye Kongamano Hilo Na Kuyafanyia Kazi Kwa Kuwa Ni Fursa Ya
Kipekee Kwao Itakayowasaidia Kuwafungua Kifikra Na Hatimaye Kujiajiri.
Akitoa Wasilisho Kuhusu Programu
Ya Mining For A Brighter Tomorrow (MBT), Kamishna Msaidizi Wa Madini Anayeshughulikia
Ushiriki Wa Watanzania Kwenye Miradi Ya Madini (Local Content) Pamoja Na Wajibu
Wa Kampuni Kwa Jamii (CSR) Maruvuko Msechu Amesema Kuwa Programu Hiyo
Imeandaliwa Na Wizara Ya Madini Kwa Lengo La Kuhakikisha Makundi Ya Wanawake Na
Vijana Yanafaidika Na Rasilimali Madini Yaliyopo Nchini.
Amesema Kuwa, Kupitia MBT,
Wizara Inalenga Kuwapatia Vijana Na Wakinamama Kwenye Vikundi Leseni Katika
Maeneo Ya Uchimbaji Pamoja Na Wachimbaji Kunufaika Na Vitendea Kazi Ikiwemo
Magari, Vifaa Na Mitambo Ya Uchimbaji.
Ameongeza Kuwa, Matarajio
Ya Programu Ni Kuchochea Ukuaji Wa Sekta Ya Madini, Kuongeza Ajira Kwa Watanzania,
Kuwajengea Uwezo Vijana Katika Kushiriki Kwenye Uchumi Wa Madini Na Uwekezaji
Katika Sekta Ya Madini, Ushiriki Kwa Vijana Kwenye Maamuzi Na Usimamizi Wa Sheria,
Pia, Msechu Amesema Kuwa MBT
Inatarajiwa Kuongeza Ushiriki Wa Watanzania Katika Shughuli Za Madini Na Uwajibikaji
Wa Kampuni Kwa Jamii, Kuwajengea Uwezo Vijana Na Wanawake Wa Tanzania Kwenye
Biashara Ya Madini Kupitia Fursa Za Uwepo Wa Madini Ya Aina Mbalimbali Tanzania.