MAHAKAMA Ya
Wilaya Bukoba Mkoani Kagera Imemtia Hatiani Mzabuni,Consolatha John Balole Ambaye
Ni Meneja Wa Kampuni Ya Zainabbas Enterprises.
Mshtakiwa Ametiwa Hatiani
Na Kuamriwa Alipe Faini Ya Shilingi 500,000 Au Kutumikia Kifungo Cha Miaka
Mitatu Jela, Kwa Kosa La Hongo Alilolitenda Kinyume Na Kifungu Cha 15 (1) (A)
Na (B) PCCA.
Hukumu Hiyo Dhidi Ya Consolatha
John Balole Katika Shauri La Rushwa Namba 13177/2024 Imetolewa Mei 17,2024 Na Mheshimiwa
Hakimu Flora Kaijage Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Bukoba.
Ilidaiwa Kwamba Kati Ya
Mwezi Machi Na Septemba,2022 Mshitakiwa Alijipatia Manufaa Isivyo Stahili Hongo
Ya Shilingi Milioni 15. 54
Katika Manunuzi Ya Vifaa
Vya Ujenzi Wa Nyumba Ya Makazi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Kagera, Fedha Ambayo
Amekwisharejesha Katika Ofisi Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Kagera.
Hata Hivyo, Mshtakiwa
Amelipa Faini Na Kuachiwa Huru.