RAIS Wa Shirikisho La
Soka Afrika (Caf), Patrice Motsepe Amekiri Kuwa Goli La Yanga Lililokataliwa
Mwamuzi Katika Mchezo Wa Robo Fainali Dhidi Ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini
Lilikuwa Goli Halali.
Rais Motsepe Ameyasema Hayo Leo Alipowasili Visiwani Zanzibar Katika Fainali Za
African Schools Football Na Kupokelewa Na Mwenyeji Wake Rais Wa Tff Wallace
Karia.
“Japo Rais Wa Caf Hatakiwi Kutoa Maoni Yoyote Kuhusu Maamuzi Ya Mwamuzi Lakini
Kwangu Mimi Nilivyorudia Kuangalia Lilikuwa Ni Goli Halali” — Amesema Motsepe.
Goli Hilo Lilifungwa Na Kiungo Wa Yanga Stephen Aziz Ki Ambapo Mwamuzi
Alilikataa Kwa Kile Alichoamini Mpira Haukuvuka Mstari Wa Goli.
Tags
SPORTS