MGOMO Wa Wafanyabiashara
Katika Soko La Mwanjelwa Jijini Mbeya, Umeendelea Tena Leo Baada Ya Maduka
Kutofunguliwa.
Mgomo Huo Ulioanza Jana Mei 23, Unafanywa Na Wafanyabiashara Wanaodai Kuwapo
Utitiri Wa Kodi Kutoka Mamlaka Ya Mapato Tanzania (Tra), Manyanyaso, Kukamatwa
Kwa Mizigo Yao Na Kufungiwa Maduka Na Halmashauri Ya Jiji La Mbeya Pindi
Wanapochelewesha Malipo Ya Huduma Kwa Wateja.
Mwananchi Digital Imefika Asubuhi Ya Leo Mei 24, 2024 Katika Soko Hilo Kubwa
Jijini Hapa Na Kushuhudia Maduka Yakiwa Yamefungwa, Huku Wafanyabiashara Wakiwa
Katika Makundi Wakiendelea Na Maongezi Binafsi.
Hata Hivyo, Habari Ambazo Hazijawa Rasmi Kutoka Kwa Wafanyabiashara, Zinaeleza
Kuwa Mgomo Huo Utadumu Kwa Siku Mbili Wakati Wakisubiri Hatma Ya Kilio Chao
Kama Kitasikika Kwa Serikali.
Mmoja Wa Wafanyabiashara Ambaye Hakutaja Majina Yake, Amesema Kwa Sasa
Wanasubiri Tamko La Viongozi Wao Kujua Lini Wataanza Kutoa Huduma.
"Leo Tumeambiwa Kutakuwapo Na Mkutano Kwa Hiyo Tupo Hapa Tunasubiri Huenda
Viongozi Wetu Wapo Kwenye Kikao Ili Baadaye Watuite, Hatufungui Hadi Tutakapopewa
Maelekezo," Amesema.
Endelea Kufuatilia Mwananchi Na Mitandao Yetu Kwa Habari Zaidi.
Tags
BUSINESS