KOCHA Wa Manchester City,
Pep Guardiola Jana Alimwaga Machozi Baada Ya Kuulizwa Swali Kuhusu Kuondoka Kwa
Meneja Wa Liverpool, Jurgen Klopp.
Klopp Jana Aliiongoza Liverpool
Kwenye Mchezo Wa Mwisho Na Kuachana Na Timu Hiyo, Akiwa Anasema Kuwa Anataka
Kwenda Kupumzika.
Guardiola Aliiongoza City
Kutwaa Ubingwa Wa Sita Ndani Ya Misimu Saba Jana Baada Ya Timu Yake Kuibuka Na
Ushindi Wa Mabao 3-1 Dhidi Ya West Ham Ambapo Timu Yake Ilifikisha Pointi 91
Mbili Mbele Ya Arsenal Iliyomaliza Nafasi Ya Pili.
"Nitammisi Sana, Jurgen
Amekuwa Mtu Muhimu Sana Kwenye Maisha Yangu Ya Soka, Amenifanya Niwe Kwenye
Levo Nyingine Kwenye Maisha Yangu.
"Nafikiri Tunaheshimiana
Kila Siku Na Ni Mtu Wangu Wa Karibu Sana, Naona Bado Anaweza Kurudi, Nataka
Kumshukuru Sana Kwa Maneno Yake," Alisema Guardiola Huku Akifuta Machozi.
Ijumaa Iliyopita, Klopp Alisema
Guardiola Ndiye Kocha Bora Zaidi Duniani Kwa Sasa Jambo Ambalo Waandishi Walimuuliza
Pep Anajisikiaje Baada Ya Kauli Hiyo.
Klopp Ambaye Ameshatwaa Ligi Ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu Ya England Na Klabu Bingwa Dunia Amemaliza Msimu Wa Mwisho Timu Yake Ikishika Nafasi Ya Tatu Pointi Tisa Nyuma Ya Vinara Manchester City.