WAKATI Taratibu Za
Mazishi Ya Rais Wa Iran, Ebrahim Raisi Zikiendelea, Makamu Wa Rais Mohammad
Mokhber Anayetarajiwa Kurithi Nafasi Hiyo Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Nchi Hiyo,
Ameongoza Mkutano Wa Dharura Wa Baraza La Mawaziri.
Raisi Amefariki Kwenye
Ajali Ya Helikopta Jana Mei 19, 2024 Akiwa Pamoja Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa
Nchi Hiyo Hossein Amir-Abdollahian Ambaye Pia Amefariki Dunia Wakati Walipokuwa
Wakirejea Kutoka Nchi Jirani Ya Azerbaijan Kwenye Hafla Ya Uzinduzi Wa Bwawa.
Ajali Hiyo Imetokea Eneo
La Milimani Katika Jimbo La East Azerbaijan, Ambapo Pia Ndani Ya Helkopta
Walikuwa Pamoja Na Gavana Wa Mkoa Wa Azerbaijan Mashariki, Malek Rahmati Wa Iran
Na Mwakilishi Wa Kiongozi Wa Mapinduzi Ya Kiislamu Katika Mkoa Wa Azerbaijan
Mashariki, Ayatollah Mohammad Ali Ale-Hashem Pamoja Na Walinzi.
Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Iran,
Iwapo Rais Atafariki Akiwa Madarakani, Kifungu Cha 131 Kinasema Makamu Wa
Kwanza Wa Rais Ndiye Atakayeshika Madaraka, Huku Baraza Linalojumuisha Makamu
Wa Kwanza Wa Rais, Spika Wa Bunge Na Mkuu Wa Mahakama Lazima Lipange Uchaguzi
Wa Rais Mpya Ndani Ya Muda Usiozidi Siku 50.
Rais Mpya
Makamu Wa Rais Mohammad
Mokhber Anatarajiwa Kuwa Rais Wa Mpito Wa Nchi Hiyo, Ambaye Atasaidia Kuandaa
Uchaguzi Wa Rais Ambao Unapaswa Kufanyika Ndani Ya Siku 50 Baada Ya Kifo Cha
Rais.
Kwa Mujibu Wa Shirika La
Habari La Reuters, Mokhber Aliyezaliwa Septemba 1, 1955, Anaonekana Kuwa Karibu
Na Kiongozi Mkuu Ali Khamenei, Ambaye Ana Kauli Ya Mwisho Katika Masuala Yote
Ya Serikali. Mokhber Alikua Makamu Wa Kwanza Wa Rais Mwaka 2021 Wakati Raisi Alipochaguliwa
Kuwa Rais.
Mokhber Alikuwa Sehemu Ya
Timu Ya Maofisa Wa Iran Ambao Walitembelea Moscow Oktoba, 2023 Na Walikubaliana
Kusambaza Makombora Ya Ardhini Hadi Ardhini Na Droni Zaidi Kwa Jeshi La Russia.
Timu Hiyo Pia Ilijumuisha
Maofisa Wawili Wakuu Kutoka Walinzi Wa Mapinduzi Ya Iran Na Ofisa Kutoka Baraza
Kuu La Usalama Wa Taifa.
Mokhber Hapo Awali
Alikuwa Mkuu Wa Mfuko Wa Uwekezaji Unaohusishwa Na Kiongozi Mkuu (Setad).
Mnamo Mwaka 2010, Umoja Wa
Ulaya Ulimjumuisha Mokhber Kwenye Orodha Ya Watu Na Mashirika Yanayowekewa
Vikwazo Kwa Madai Ya Kuhusika Katika "Shughuli Za Nyuklia Au Za Makombora
Ya Ballistic". Miaka Miwili Baadaye, Walimwondoa Kwenye Orodha Hiyo.
Mnamo Mwaka 2013, Idara Ya
Hazina Ya Marekani Iliongeza Setad Na Kampuni 37 Ambazo Ilizisimamia Kwenye Orodha
Ya Mashirika Yaliyowekewa Vikwazo.
Setad, Jina Lake Kamili
Ni Setad Ejraiye Farmane Hazrate Emam, Au Makao Makuu Ya Kutekeleza Amri Ya Imamu,
Ilianzishwa Chini Ya Amri Iliyotolewa Na Mwanzilishi Wa Jamhuri Ya Kiislamu,
Mtangulizi Wa Khamenei, Ayatollah Ruhollah Khomeini.
Ilielekeza Wasaidizi
Kuuza Na Kusimamia Mali Ambazo Zinadaiwa Kutelekezwa Katika Miaka Ya Machafuko
Baada Ya Mapinduzi Ya Kiislamu Ya Mwaka 1979 Na Kuelekeza Sehemu Kubwa Ya
Mapato Hayo Kwa Misaada.
Salamu Za Rambirambi
Baada Ya Kutokea Msiba
Huo, Viongozi Na Taasisi Mbalimbali Duniani Wamekuwa Wakitoa Salamu Za
Rambirambi. Miongoni Mwao Ni Kundi La Hamas Ambalo Limetoa Taarifa Ikimshukuru
Rais Wa Iran Ebrahim Raisi Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Hossein Amir-Abdollahian Kwa
Msaada Wao Katika Vita Vyake Dhidi Ya Israel Baada Ya Vifo Vyao Jana.
“Viongozi Hawa Waliunga
Mkono Mapambano Halali Ya Watu Wetu Dhidi Ya Chombo Cha Kizayuni, Walitoa
Msaada Wa Thamani Kwa Upinzani Wa Palestina, Na Walifanya Jitihada Zisizochoka
Katika Mshikamano Na Msaada Katika Mabaraza Na Nyanja Zote Kwa Watu Wetu Katika
Ukanda Wa Gaza Unaosimama Imara. Pia Walifanya Juhudi Kubwa Za Kisiasa Na
Kidiplomasia Kusimamisha Uchokozi Wa Kizayuni Dhidi Ya Watu Wetu Wa Palestina,”
Imesema Taarifa Ya Hamas.
Kwa Upande Mwingine, Rais
Wa Baraza La Ulaya, Charles Michel, Alisema Asubuhi Hii Kwamba "EU Inaeleza
Rambirambi Zake Za Dhati Kwa Kifo Cha Rais Ebrahim Raisi Na Waziri Wa Mambo Ya
Nje Hossein Amir-Abdollahian, Pamoja Na Wanachama Wengine Wa Ujumbe Wao Na
Wafanyakazi Katika Ajali Ya Helikopta."
Ubalozi Wa Russia Huko Tehran
Pia Umetuma Rambirambi Zake Siku Ya Jumatatu Kufuatia Kifo Hicho, Ikimlilia Raisi
Aliyeisambazia Urusi Silaha Kwa Ajili Ya Matumizi Katika Uvamizi Wake Wa Ukraine.
“Fikra Zetu Ziwaendee
Familia,” Aliongeza. Ubalozi Wa Russia Huko Tehran.
Kwa Upande Wake Rais Wa Umoja
Wa Falme Za Kiarabu (UAE), Mohammed Bin Zayed Al Nahyan, Amesema Nchi Yake
Inasimama Kwa Mshikamano Na Iran Katika Kile Alichokiita "Wakati
Mgumu," Na Kutoa Rambirambi Kwa Serikali Ya Iran Na Watu Wa Iran.
Marais Waliokufa Katika
Ajali Za Ndege
Miongoni Mwa Marais
Waliowahi Kufariki Kutokana Na Ajali Za Ndege Ni Pamoja Aliyewahi Kuwa Rais Wa Paraguay,
José Félix Estigarribia, Aliyefariki Septemba 7, 1940 Altos, Paraguay, Baada Ya
Ndege Aina Ya Potez 25 Kuanguka.
Mwingine Ni Aliyekuwa Rais
Wa Ufilipino, Ramon Magsaysay, Aliyefariki Machi 17, 1957 Katika Mlima Balamban,
Cebu Baada Ya Ndege Aina Ya Douglas C-47 Skytrain Kupata Ajali.
Nate Rais: Nereu Ramos Wa
Brazil Alifariki Juni 16, 1958 São José Dos Pinhais, Brazil Baada Ya Ndege Aina
Ya Douglas C-47 Skytrain Kupata Ajali. Pia Katika Orodha Hiyo Yumo Aliyekuwa Rais
Wa Iraq, Abdul Salam Arif Aliyefariki Aprili 13, 1966 Baghdad, Iraq Baada Ya
Ndege Aina Ya De Havilland Dove Kupata Ajali.
Julai 18, 1967 Pia
Ilitokea Ajali Ya Ndege Aina Ya Piper PA-23 Na Kupoteza Maisha Ya Aliyekuwa Rais
Wa Brazil, Castelo Branco. Aliyekuwa Rais Wa Bolivia, René Barrientos,
Alifariki Kwenye Ajali Ya Ndege Aprili 27, 1969.
Aliyekuwa Rais Wa Ecuador,
Jaime Roldós Aguilera Naye Alifariki Kwenye Ajali Ya Ndege Mei 24, 1981 Maeneo
Ya Huairapungo, Ecuador
Oktoba 19, 1986, Ilitokea
Ajali Ya Ndege Katika Maeneo Ya Mbuzini Nchini Afrika Kusini Msumbiji Na
Kusababisha Kifo Cha Rais Samora Machel Wa Msumbiji.
Agosti 17, 1988 Pia
Ilitokea Ajali Ya Ndege Maeneo Ya Bahawalpur Ndhini Pakistan Iliyopoteza Maisha
Ya Aliyekuwa Rais Wan Chi Hiyo, Muhammad Zia-Ul-Haq.
Aprili 6, 1994, Aliyekuwa
Rais Wa Rwanda Juvénal Habyarimana Na Mwenzake Cyprien Ntaryamira Wa Burundi Walifariki
Kwenye Ajali Ya Ndege Aina Ya Dassault Falcon 50 Iliyokuwa Ikitokea Dar Es Salaam
Ikielekea Kigali.
Mwingine Ni Aliyekuwa Rais
Wa Macedonia Kaskazini, Boris Trajkovski Alifariki Kwa Ajali Ya Ndege
Iliyotokea Februari 26, 2004 Mostar, Bosnia Na Herzegovina. Vilevile Aliyekuwa Rais
Wa Poland, Lech Kaczyński Alifariki Kwa Ajali Ya Ndege Aprili 10, 2010
Iloiyotokea Nchini Russia, Huku Aliyekuwa Rais Wa Chile, Sebastián Piñera Akifariki
Kwa Ajali Ya Ndege Iliyotokea Ziwa Ranco Nchini Humo, Chile Februari 6, 2024.