WIZARA Ya Afya Inayosimamiwa Na Hamas Huko Gaza Imesema Makumi Ya Watu Waliuawa Au Kujeruhiwa Katika Mlipuko Katika Kambi Ya Wakimbizi Katika Eneo La Rafah.
Jeshi La Ulinzi La Israel (IDF) Limesema Limefanya Shambulizi La Anga Likilenga Makao Ya Hamas Katika Eneo Hilo. Inasema Inafanyia Uchunguzi Tukio Hilo.
Mapema Siku Hiyo Hamas Ilirusha Makombora Manane Kutoka Rafah Kuelekea Tel Aviv, Ikiwa Ni Mashambulizi Ya Kwanza Ya Masafa Marefu Katika Mji Huo Tangu Januari.
Video Kutoka Kusini Mwa Ukanda Wa Gaza Zinaonesha Mlipuko Mkubwa Na Moto Mkali Ukiwaka.
Hamas Imesema Mashambulizi Ya Anga Ya Israel Yamepiga Kambi Ya Wapalestina Waliokimbia Makazi Yao Kaskazini-Magharibi Mwa Rafah, Mbali Na Operesheni Za Hivi Karibuni Za Kijeshi Katika Eneo Lililotengwa La Usalama La Kibinadamu.
Inasema Wanawake Na Watoto Ni Miongoni Mwa Waliofariki.
IDF Ilisema Iliwalenga Wanamgambo Wa Hamas Katika Eneo Hilo Na Ikasema Inafahamu Ripoti Kwamba Shambulio Hilo Lilisababisha Moto Ambao Uliwadhuru Raia.
Ilikuwa Inachunguza Hilo Lakini Ilisema Imetumia Silaha Za Usahihi Dhidi Ya Maeneo Halali Ya Shabaha.
Mapema Siku Ya Jumapili Ving'ora Vya Mashambulizi Ya Anga Vilisikika Karibu Na Tel Aviv Wakati Israel Iliposhambuliwa Na Roketi Za Hamas, Zilizorushwa Kutoka Karibu Na Rafah.
Roketi Hizo Nane Ama Zilinaswa Na Mifumo Ya Ulinzi Wa Anga Au Zilianguka Uwanjani.
Mashambulizi Ya Kijeshi Ya Israel Yameendelea
Huko Rafah, Licha Ya Mahakama Ya Kimataifa Ya Haki Kutoa Uamuzi Siku Ya Ijumaa Kwamba
Lazima Ikomeshwe.