KOCHA wa Ipswich Town,
Kieran McKenna, ambaye amekuwa akihusishwa na Brighton na Chelsea, atasubiri
klabu ya zamani ya Manchester United, ambako aliwahi kufanya kazi kama
mkufunzi, kabla ya kuamua uhamisho wake mwingine. (Time)
Manchester United
itamfuta kazi meneja Erik ten Hag bila kujali matokeo ya fainali ya Kombe la FA
dhidi ya Manchester City Jumamosi. (Guardian)
Vilabu vya AC Milan na
Saudi Arabia vinamfuatilia beki wa Brazil Emerson Royal, huku Tottenham
wakitafuta kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)
Kiungo mkongwe wa Croatia
Luka Modric, 38, atasaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu ya Real Madrid
baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Relevo)
AC Milan na Juventus wana
nia ya kumsajili mlinzi wa Borussia Dortmund na Ujerumani Mats Hummels, 35, kwa
uhamisho wa bila malipo. (Bild)
Mauricio Pochettino
angependa kusalia katika Ligi ya Premia baada ya kuondoka Chelsea na huenda
akavutiwa na kazi ya Manchester United ikiwa wataachana na Ten Hag. (Standard)
Borussia Dortmund wanatarajiwa
kufanya mazungumzo kuhusu kubadilisha mkataba wa mkopo wa winga wa Manchester
United Jadon Sancho kuwa wa kudumu baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
lakini uwezekano wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hauonekani
kutokana na bei ya klabu hiyo ya Old Trafford kuwa juu sana. (Sky Sports )
Bayern Munich itampa
kocha wa Burnley Vincent Kompany kandarasi hadi 2027 ili kuwa meneja wao mpya,
huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiwa katika awamu ya mwisho ya mazungumzo na
Clarets kuhusu kumwajiri Mbelgiji huyo. (Sky Sports )
Gian Piero Gasperini
anakaribia kunyima nafasi ya kuwa kocha wa Napoli na kusaini mkataba mpya na
Atalanta baada ya kushinda Ligi ya Europa. (L’Eco di Bergamo kupitia Football
Italia)
Vilabu vya Saudi Arabia
viko tayari kusubiri hadi msimu ujao wa joto kujaribu kumsajili mshambuliaji wa
Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 31, na kiungo wa kati wa Manchester City
na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 32, kwa uhamisho wa bure ikiwa hawatawapata wawili
hao msimu huu. (Telegraph )
Chelsea wanatarajiwa
kufanya mazungumzo na kocha wa Leicester City Enzo Maresca wakati wakiendelea
na harakati zao za kutafuta mrithi wa Pochettino. (Standard)
Kipengele cha kuachiliwa kwa
Maresca katika mkataba wake Leicester kinaaminika kuwa takribani pauni milioni
7.5. (Talksport)
Chelsea haijaondoa
uwezekano wa kumnunua Roberto de Zerbi, ambaye aliondoka Brighton kwa
makubaliano mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)