PICHA Zilizopatikana Na CNN
Wiki Hii Zinaonyesha Combs - Anayejulikana Pia Kama P Diddy Na Puff Daddy -
Akimpiga Ngumi Na Mateke Cassie Kwenye Barabara Ya Ukumbi Ya Hoteli Ya Los
Angeles Mnamo 5 Machi 2016.
Sean "Diddy" Combs
Anachukua "Wajibu Kamili" Kwa Tabia Yake Iliyoonyeshwa Kwenye Video
Iliyoibuka Hivi Majuzi Ya 2016 Ambapo Mwanamuziki Huyo Na Nguli Anamshambulia
Mpenzi Wake Wa Wakati Huo, Mwimbaji Cassie Ventura, A.K.A. Cassie.
"Ni Ngumu Sana
Kutafakari Nyakati Za Giza Zaidi Maishani Mwako, Lakini Wakati Mwingine Lazima
Ufanye Hivyo," Combs Alisema Kwenye Video Mpya Aliyoituma Kwa Instagram
Jumapili, Siku Mbili Baada Ya Video Iliyopatikana Kwa Mara Ya Kwanza Na CNN Kutolewa
Kwa Umma. "Nilikuwa Na --- Nimechoka. Yaani Niligonga Mwamba. Lakini Sitoi
Visingizio. Tabia Yangu Kwenye Video Hiyo Haina Udhuru.”
Katika Picha Hiyo Ya
Uchunguzi Ambayo Haina Sauti, Combs Anaonekana Akikimbia Kwenye Barabara Ya
Ukumbi Wa Hoteli Akiwa Amevalia Taulo Na Soksi, Akimkimbiza Ventura Huku
Akisubiri Lifti Kisha Akamshika Shingoni Na Kumtupa Chini. Kisha Anaonyeshwa
Akimpiga Teke Huku Akiwa Amejikunja Chini, Akimburuta Kutoka Eneo Moja Hadi
Jingine, Na Baadaye Kumsukuma Na Kumrushia Kitu.