JESHI LA POLISI Mkoani Simiyu
Linawashikilia Watu Wanane Kwa Tuhuma Za Kukamatwa Na Dawa Za Kulevya Kati Ya
Watuhumiwa Mia Moja Arobaini Na Nane Katika Kipindi Cha Mwezi April Mwaka Huu.
Akizungumza Na Waandishi
Wa Habari Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Simiyu,Kamishina Msaidizi Wa
Polisi(ACP) Edith Swebe Amesema Kuwa Katika Kipindi Cha Mwezi April Jeshi La
Polisi Walifanya Oparesheni Ya Kukamata Dawa Za Kulevya Na Kufanikiwa Kukamata
Watuhumiwa Wanane Pamoja Na Magari Manne Ambayo Yalikuwa Yanatumika
Kusafirishia Katika Wilaya Za Maswa Na Busega Mkoani Hapo.
Sauti Ya ACP Edith Swebe Akielezea
Walivyofanikiwa Kukamata Watuhumiwa Wa Dawa Za Kulevya
Swebe Ameongeza Kuwa
Katika Kipindi Cha Mwezi April Walifanikiwa Kukamata Watuhumiwa Mia Moja Na
Arobaini Na Nane Kwa Matukio Mbalimbali Yakiwezo Wizi,Ujangili Na Madawa Ya
Kulevya.
Sauti Ya ACP Edith Swebe Akizungumzia
Mafanikio Ya Oparesheni
Katika Hatua Nyingine ACP
Edith Swebe Ametoa Wito Kwa Wananchi Mkoani Hapo Kuacha Kujihusisha Na Matukio
Ya Kihalifu Ambayo Yanayoweza Kuwaweka Katika Mikono Ya Jeshi La Polisi
Huku Akiwaomba Wananchi Kuendelea Kutoa Ushirikiaano Ili Kukomesha Vitendo Vya
Uhalifu.