UINGEREZA Inaweza Kumteua
Meneja Wa Zamani Wa Chelsea Mauricio Pochettino Ikiwa Gareth Southgate Ataondoka
Wadhifa Wake Baada Ya Euro 2024. (Telegraph - Usajili Unahitajika)
Muargentina Pochettino,
52, Angependa Kuzungumza Na Manchester United Iwapo Watamfuta Kazi Meneja Erik Ten
Hag (Times)
Chelsea Imeunda Orodha
Fupi Ya Wagombea Wanaopigiwa Upatu Kuchukua Nafasi Ya Pochettino Na Wanatarajia
Kufanya Uteuzi Baada Ya Siku Chache (Athletic)
Klabu
Mpya Iliyopanda Daraja Inajaribu Kumshawishi Meneja Wao Kusalia, Wakati Mauricio
Pochettino Akiwa Na Chaguzi Kadhaa Mezani Za Kuamua Atakokwenda..
Ipswich Imempa Meneja KieranMckenna
Mkataba Mpya Ulioboreshwa Kwa Matumaini Ya Kusalia Naye Huku Kukiwa Na Nia Ya Manchester
United , Chelsea Na Brighton Kumchukua (Sun),
Chelsea Wako Kwenye
Mazungumzo Na Wawakilishi Wa Mckenna Kuhusu Kocha Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 38
Kuwa Meneja Wao Mpya. (Football Insider)
Kiungo Wa Kati Wa Ureno
Bernardo Silva, 29, Anaweza Kuondoka Msimu Huu Ikiwa Manchester City Itapokea
Ofa Ya Takriban £50m. (Football Insider)
Mshambulizi Wa Napoli Na Nigeria
Victor Osimhen, 25, Anatazamiwa Kukataa Ofa Kutoka Klabu Za Paris St-Germain Na
Saudi Arabia Huku Akitarajia Kuhamia Chelsea(Teamtalk)
Tottenham Wako Tayari
Kumuuza Mshambuliaji Wa Brazil Richarlison, 27, Ili Kutoa Nafasi Kwa
Mshambuliaji Wa Uingereza Na Bournemouth Dominic Solanke, 26. (Talksport)
Kipa Wa England Jordan
Pickford, 30, Ametoa Ishara Za Wazi Kwamba Atasalia Na Everton Licha Ya
Kuivutia Chelsea.(Mirror)
Mkurugenzi Wa Michezo Wa Crystal
Palace Dougie Freedman, 49, Amekataa Ofa Kutoka Kwa Newcastle United Kuchukua
Nafasi Ya Dan Ashworth Katika Nafasi Kama Hiyo Na Atasalia Na The Eagles. (Football
Insider)
Mshambulizi Wa Slovenia
Benjamin Sesko, 20, Ambaye Yuko Kwenye Rada Ya Chelsea Na Arsenal , Ataamua
Kabla Ya Michuano Ya Euro Ikiwa Anataka Kusalia RB Leipzig Au Kuondoka. (Fabrizio
Romano)
Newcastle Wanakaribia
Kuwasajili Wachezaji Wawili Wa Safu Ya Ulinzi Ya Uingereza Tosin Adarabioyo,
26, Na Lloyd Kelly, 25, Ambao Watakuwa Wachezaji Huru Wakati Mikataba Yao
Katika Klabu Ya Fulham Na Bournemouth Itakapotamatika Msimu Huu, Huku Eddie
Howe Pia Akimtaka Fowadi Wa Crystal Palace Michael Olise, 22, Ingawa Mchezaji Huyo
Wa Kimataifa Wa Ufaransa Wa Kikosi Cha Wachezaji Chini Ya Miaka 21 Anamezewa
Mate Na Vilabu Vingi(Teamtalk)
Wawakilishi Wa Mchezaji
Wa Manchester City Kevin De Bruyne Walifanya Mazungumzo Na Klabu Mpya Ya MLS
San Diego FC , Lakini Hakuna Daalili Kwamba Kiungo Huyo Wa Kati Wa Ubelgiji,
32, Yuko Tayari Kuhama(Athletic)
Arsenal Wako Tayari
Kumnunua Kipa Wa Feyenoord Na Uholanzi Justin Bijlow, 26, Huku Wakitarajia
Mlinda Lango Wao Wa England Aaron Ramsdale, 26, Kuondoka.(Mirror)
Crystal Palace Wameafikiana Na Beki Wa Kati Wa Morocco Na Real Betis Chadi Riad, 20, Katika Mkataba Wa Thamani Ya Hadi £14m(Standard)