MAMLAKA Ya Hali Ya Hewa
Tanzania (TMA) Imesema, Kwa Sasa Hakuna Tena Tishio La Kimbunga Ialy Katika
Nchi Hiyo Ya Afrika Mashariki.
Taarifa Ya TMA Kwa Ummya
Waliyoitoa Saa 4:00 Usiku Wa Jana Jumatano, Mei 22, 2024 Ilisema Wanahitimisha
Mfululizo Wa Taarifa Za Kilichokuwa Kimbunga Ialy Zilizokuwa Zikizitoa Tangu Mei
17, 2024.
"Mwenendo Wa Mifumo
Ya Hali Ya Hewa Unaonesha Katika Kipindi Cha Saa 6 Zilizopita, Kimbunga Ialy Kimepoteza
Kabisa Nguvu Yake, Kikiwa Kaskazini Mashariki Mwa Pwani Ya Kenya.
"Hivyo, Kwa Sasa
Hakuna Tena Tishio La Kimbunga Ialy Katika Nchi Yetu," Amesema.
Aidha, Wakati Kikipita
Karibu Na Pwani Na Nchi Yetu Kati Ya Juzi Jumanne Mei 21 Na Leo Tarehe 22 Mei 2024
Kimeweza Kusababisha Vipindi Vya Mvua, Upepo Mkali Na Mawimbi Makubwa Katika
Maeneo Ya Pwani Ya Nchi Yetu Kama Ilivyotabiriwa Awali.
"Hata Hivyo,
Ikumbukwe Japo Tunaelekea Mwishoni Mwa Msimu Wa Masika, 2024, Tunakaribia
Kuanza Kwa Msimu Wa Kipupwe, Na Kwasababu Hiyo, Vipindi Vya Upepo Wa Kusi Baharini
Vinaweza Kuanza Kujitokeza Na Kuambatana Na Mawimbi Makubwa Kwa Baadhi Ya
Nyakati," Imeeleza Taarifa Hiyo.
TMA Imewashauri Wananchi
Na Watumiaji Wa Bahari Kuendelea Kufuatilia Na Kuzingatia Taarifa Za Utabiri
Kutoka Mamlaka Ya Hali Ya Hewa Tanzania Pamoja Na Maelekezo Na Miongozo
Inayotolewa Na Mamlaka Husika.