MANCHESTER UNITED Wanataka
Takriban Asilimia 75 Ya Pauni Milioni 75 Walizolipa Borussia Dortmund Kwa Winga
Wa Uingereza Jadon Sancho, 24, Ambaye Atahitaji Kupunguzwa Mshahara Wake Wa
Pauni 275,000 Kwa Wiki Ikiwa Klabu Hiyo Ya Bundesliga Itakamilisha Dili La
Kumsaini Tena(Sun)
Mkufunzi Wa Chelsea
Mauricio Pochettino Anasema Atafurahi Kuhifadhi 80-85% Ya Kikosi Chake Msimu
Ujao(Football.London)
Mwenyekiti Mwenza Wa Arsenal
Josh Kroenke Amewaambia Mashabiki "Klabu Haitasimama Tuli"
Inapotafuta Wachezaji Ili Kusaidia Kupata Taji La Uingereza Na Ulaya(Goal)
West Ham Wanakaribia
Kumsajili Mlinzi Mwenye Umri Wa Miaka 18 Mwingereza Luis Brown Kutoka Arsenal(Caught
Offside)
RB Leipzig Wamempa
Mshambuliaji Wa Slovenia Benjamin Sesko Mwenye Umri Wa Miaka 20 - Ambaye
Anahusishwa Na Kuhamia Arsenal - Nyongeza Ya Muda Wa Kandarasi Ya Mwaka Mmoja.
(Fabrizio Romano)
Kipa Wa Uhispania David
Raya, 28, Anasema Hajafanya Mazungumzo Yoyote Na Arsenal Kuhusu Iwapo Watafanya
Uhamisho Wake Wa Mkopo Kutoka Brentford Kuwa Wa Kudumu. (Express)
Meneja Wa Tottenham Ange
Postecoglou Ataweka Kipaumbele Kumsaini Mshambuliaji Mpya Na Kiungo Wa Safu Ya
Ulinzi Huku Akipanga Kuwaachilia Wachezaji Wengi Msimu Wa Joto (Mirror)
Ipswich Wanasema
Wanafanya Kila Linalowezekana Kusalia Na Meneja Kieran Mckenna Huku Kukiwa Na
Nia Ya Kumchukua Kocha Huyo Kutoka Kwa Brighton , Chelsea Na Manchester United .(Teamtalk)
Sheffield United Ingelazimika
Kulipa Kiasi Cha Tarakimu Sita Kwa Kiungo Wa Kati Wa Brazil Vinicius Souza Kwa
Klabu Ya Zamani Ya Lommel Iwapo Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 24 Angeanza
Katika Mechi Dhidi Ya Tottenham Jumapili (Sun)
Bayern Munich Na Ajax Wanaendelea
Kupigania Sahihi Ya Erik Ten Hag, 54, Kwa Imani Kwamba Atafutwa Kazi Kama
Meneja Wa Manchester United Mwishoni Mwa Msimu Huu(Mirror)