MTU MMOJA Amethibitishwa
Kufariki Huku Wengine Wakipata Majeraha Tofauti Tofauti Kufuatia Ajali
Iliyohusisha Magari Kadhaa Ya Msafara Wa Rais Nana Akufo Addo Siku Ya Jumapili.
Chanzo Kamili Cha Ajali
Hiyo Hakijajulikana.
Msafara Huo Ulikuwa
Ukirejea Kutoka Kumasi Kuelekea Mji Mkuu, Accra.
Dereva Wa Mojawapo Ya
Magari Hayo Alipoteza Maisha, Huku Wengine Katika Usalama Wa Rais Wakipata
Majeraha Mbalimbali Na Wamepata Matibabu Ya Awali Katika Hospitali Iliyo
Karibu.
Wamesafirishwa Hadi Accra
Kwa Matibabu Zaidi.
Baadhi Ya Magari Pia
Yameharibika Kiasi Cha Kutoweza Kurekebishwa. Taarifa Iliyotolewa Na Ofisi Ya
Rais Ilionyesha Kuwa Rais Akufo Addo Yuko Salama Na Alisafiri Kurejea Accra Kwa
Helikopta Ya Kijeshi.
Barabara Kuu Ya Accra-Kumasi
Ni Ya Njia Moja, Na Ajali Hutokea Mara Kwa Mara, Mara Nyingi Husababisha Vifo.