JESHI LA UGANDA Limesema
Limemkamata Kamanda Wa Kundi La Waasi La ADF Linaloshirikiana Na Kundi
Linalojiita Dola La Kiislamu, Ambaye Ni Mtaalamu Wa Kutengeneza Mabomu
Yaliyotumiwa Na Kundi Hilo Kutekeleza Mashambulizi Mabaya.
Kamanda Huyo Anywari Al-Iraq
Ambaye Ni Raia Wa Uganda,
Alikamatwa Katika Maeneo Ya Jangwani Mashariki Mwa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Congo,
Kunakopatikana Kundi La ADF.
Katika Operesheni Ya
Kumsaka Kamnda Huyo, Watu Tisa Wakiwemo Watoto Waliokolewa Kutoka Katika Eneo
Hilo Lililopo Mkoani Ituri Mashariki Mwa DRC, Bidhaa Nyengine Za Kutengenezea
Mabomu Pia Zilipatikana Huko.
Kundi Hilo La Waasi Wa ADF
Lilianza Harakati Zake Nchini Uganda Lakini Limekuwa Na Ngome Yake Nchini Congo
Tangu Miaka Ya 90. Lilitangaza Kushirikiana Na Kundi Linalojiita Dola
La Kiislamu Mwaka 2019 Na Linatuhumiwa Kuwauwa Mamia Ya Wanavijiji Katika
Mashambulizi Ya Mara Kwa Mara Katika Miaka Ya Hivi Karibuni.