MENEJA Wa Tottenham Ange
Postecoglou Ameiomba Klabu Hiyo Takriban Wachezaji Watatu Wapya Msimu Huu Wa Joto.
(ESPN)
Manchester United Wanavutiwa
Na Mlinzi Wa Everton Muingereza Jarrad Branthwaite, 21, Na The Toffees Wanaweza
Kumnunua Beki Wa Kati Wa Galatasaray Na Colombia Davinson Sanchez, 27, Kuziba
Nafasi Yake. (Caught Offside)
Tottenham Wako Tayari
Kumuuza Mlinzi Wa Brazil Emerson Royal, 25, Huku Juventus, AC Milan Na Bayern
Munich Zikiwa Na Hamu Ya Kumnunua (Givemesport)
Newcastle Wanaweza
Kumnunua Lloyd Kelly, 25, Huku Beki Huyo Wa Uingereza Akitarajiwa Kuondoka Bournemouth
Kama Mchezaji Huru. (Fabrizio Romano)
Chelsea Itadai Ada Ya
Pauni Milioni 25 Kwa Mlinzi Wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, Ambaye
Anatarajiwa Kuvutia Vilabu Kadhaa (Telegraph)
Rais Wa Corinthians
Augusto Melo Atasafiri Hadi Uingereza Wiki Ijayo Kuzungumza Na Vilabu Kuhusu
Uwezekano Wa Kuuzwa Kwa Mshambuliaji Wa Brazil Wesley Mwenye Umri Wa Miaka 19.
(Globo Esporte - Kwa Kireno), Ya Nje
Meneja Wa Burnley Vincent
Kompany, 38, Ni Miongoni Mwa Watu Wanaopigiwa Upatu Kuchukua Nafasi Ya Thomas
Tuchel Huko Bayern Munich. (Fabrizio Romano)
Aston Villa Wanakaribia
Kufikia Makubaliano Ya Kumnunua Tena Mchezaji Wa Luton Town Na Kiungo Wa Kati
Wa Zamani Wa Uingereza Ross Barkley Kwa Mkataba Wa Kudumu, Miaka Minne Baada Ya
Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 30 Kujiunga Kwa Mkopo Kutoka Chelsea(Guardian)
Arsenal Wanataka Kusajili
Mshambuliaji Kabla Ya Ziara Yao Ya Kujiandaa Na Msimu Mpya, Huku Nyota Wa Newcastle
United Na Uswidi Alexander Isak, 24, Na Mshambuliaji Wa Ajax Na Uholanzi, Brian
Brobbey, Wakiongoza Orodha Hiyo.(Independent)
Chelsea Na Manchester
United Zote Zimewasiliana Na Mkufunzi Wa Ipswich Town Kieran Mckenna, Huku Raia
Huyo Wa Ireland Kaskazini Akiwa Katika Harakati Za Kuchukua Nafasi Ya Mauricio
Pochettino Au Erik Ten Hag. (Manchester Evening News)
Wolves Itadai Kiasi Cha
Kuvunja Rekodi Ya Klabu Cha Pauni Milioni 60 Kwa Winga Wa Ureno Mwenye Umri Wa
Miaka 24 Pedro Neto, Ambaye Analengwa Na Manchester City Na Newcastle Msimu Wa
Joto(Telegraph )
Aston Villa Wako Tayari
Kusikiliza Ofa Kwa Mlinzi Wa Brazil Diego Carlos, 31, Huku Wakitarajia Kufuata
Sheria Za Faida Na Uendelevu(Telegraph)
Mkufunzi Wa Villa Unai
Emery Anataka Kumsajili Beki Wa Barcelona Na Uruguay Ronald Araujo, 25. (Sport Kwa
Kihispania)
Stoke Wameonyesha Nia Ya
Kutaka Kumsajili Beki Wa Uingereza Conor Coady, 31, Kutoka Leicester(Teamtalk),
Leicester Wanajiandaa
Kushindana Na Vilabu Vya Ufaransa Lyon Na Brest Kumnunua Fowadi Wa Burkina Faso
Mohamed Konate, 26, Ambaye Mkataba Wake Na Klabu Ya Urusi Akhmat Grozny Unamalizika
Msimu Huu. (Football Insider)