ASKARI Polisi Watatu Wa
Kituo Cha Tunduma, Wilaya Ya Momba, Mkoani Songwe, Wamefikishwa Mahakamani Kwa
Mashitaka Ya Kuomba Na Kupokea Rushwa Kiasi Cha Shilingi Million 55.
Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Wa Songwe Imewafikisha
Askari Hao, Leo Juni 4, 2024 Katika Mahakama Ya Wilaya Ya Momba Iliyopo Eneo La
Chapwa, Mjini Tunduma.
Askari Hao Ambao Tayari Wameshafukuzwa Kazi Na Jeshi La Polisi Kabla Ya
Kukamatwa Na Takukuru Kisha Kufikishwa Mahakamani Hapo Ni Koplo Enock Marando (43),
Koplo Samson Kalebe (38), Pamoja Na Konstebo Wa Polisi Zawad Malakasuka (39).
Mbele Ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Momba, Timoth Lyon,
Mwendesha Mashitaka Wa Takukuru Mkoa Wa Songwe, Simona Mapunda, Alidai Kuwa
Washitakiwa Walitenda Makosa Hayo, Machi 7 Mwaka Huu Katika Mpaka Wa Tunduma.
Mapunda Alidai Kuwa, Siku Ya Tukio Washitakiwa Wakiwa Ni Waajiriwa Wa Jeshi La
Polisi Waliomba Rushwa Ya Shilingi Milioni 55 Ambapo Ni Kinyume Na Kifungu Cha
15 (1) Na (2) Cha Makosa Ya Rushwa Kutoka Kwa Mfanyabiashara Halima Abdallah Ambaye
Ni Mfanyabiashara Ili Wamsaidie Baada Ya Kumkamata Na Shehena Ya Vipodozi
Vilivyopigwa Marufuku.
Hakimu Lyon, Baada Ya Kusikiliza Maelelezo Ya Kesi Hiyo Ya Rushwa Namba 15094
Ya Mwaka 2024 Na Watuhumiwa Wote Kukana Kutenda Makosa Hayo Aliahirisha Shauri
Hilo Hadi Juni 18 Mwaka Huu, Ambapo Kesi Hiyo Itarudi Mahakamni Hapo Kwa Ajili
Ya Kuanza Kusikiliza Hoja Za Awali.
Hata Hivyo, Washitakiwa Hao Walikosa Dhamana Na Kurejeshwa Mahabusu Baada Ya
Wadhamini Wao Kushindwa Kukikidhi Masharti Ya Dhamana Yaliyowekwa Na Mahakama
Hiyo.
Masharti Hayo, Yalitaka Kila Mshitakiwa Kuwa Na Wadhamini Wawili Wenye Mali
Zisizohamishika Zenye Thamani Ya Shilling Million 22.5 Kila Mmoja Wao, Pamoja
Na Washitakiwa Hao Kutakiwa Kuwasilisha Dhamana Ya Maandishi Ya Kiasi Cha
Shilling Million 19 Kila Mmoja Wao.