OMBI
La Manchester United Haliwezekani Na Real Madrid Wanaongoza Katika
Kinyang'anyiro Cha Kumsajili Yoro. (Mail)
Atletico
Madrid Wanataka Kumsajili Julian Alvarez Wa Manchester City, Manchester United
Wamejiunga Na Liverpool Katikaharakati Za Kumnasa Leny Yoro Na Galatasaray
Wanamtaka Anthony Martial.
Atletico Madrid
Wamewasiliana Na Wachezaji Watatu Wa Argentina Angel Correa, Rodrigo De Paul Na
Nahuel Molina Ili Kuuliza Kuhusu Upatikanaji Wa Mshambulizi Mwenzao,
Mshambulizi Wa Manchester City , Julian Alvarez, 24 . (Marca Kwa Kihispania)
Paris St-Germain Pia
Wanavutiwa Na Alvarez. (Fabrizio Romano)
Bayern Munich Wanataka
Kuongeza Mkataba Wa Beki Wa Pembeni Wa Canada Alphonso Davies, 23, Na Hawamtaki
Tena Beki Wa Kushoto Wa Arsenal Na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 27. (Sky
Germany)
Kiungo Mshambuliaji Wa
Fulham Wa Brazil, Andreas Pereira, 28, Anasema Atajadili Mustakabali Wake Na
Wakala Wake Baada Ya Michuano Ya Copa America Msimu Huu Wa Joto. (Uol)
Tottenham Wanataka
Kumsajili Pereira (Teamtalk)
West Ham Wametoa Ofa Ya
Pauni Milioni 6.8 Kumnunua Mlinzi Wa Brazil Vitao Mwenye Umri Wa Miaka 24
Kutoka Internacional . (Revista Colorada - Kwa Kireno)
Newcastle Wako Kwenye
Mazungumzo Ya Juu Zaidi Ya Kumsajili Beki Wa Uingereza Lloyd Kelly, 25, Ambaye
Bournemouth Wanasema Ataondoka Mwishoni Mwa Kandarasi Yake Msimu Huu Wa Joto.
Roma Na Atletico Madrid Pia Wanavutiwa Naye (Sky Sports)
Kocha Wa Zamani Wa
Chelsea Na Brighton Graham Potter Anatarajiwa Kuchukua Nafasi Ya Arne Slot Kama
Meneja Wa Feyenoord. (1908 - Kwa Kiholanzi)
Liverpool Wanalenga
Kumsajili Mlinda Lango Mpya Huku Wakijiandaa Kumruhusu Caoimhin Kelleher 25 Wa
Jamhuri Ya Ireland Kuondoka Anfield Msimu Huu Wa Joto. (Football Insider)
Tottenham , Liverpool ,
Newcastle Na West Ham Wanavutiwa Na Mlinzi Wa Feyenoord Mholanzi Lutsharel
Geertruida Mwenye Umri Wa Miaka 23. (Ad - Kwa Kiholanzi)
Manchester United
Wamejiunga Na Liverpool Katika Harakati Za Kumsaka Beki Wa Kati Wa Ufaransa
Leny Yoro Mwenye Umri Wa Miaka 18 Kutoka Lille . (Marca Kwa Kihispania)
Manchester City Wanajiandaa
Kufanya Mazungumzo Na Meneja Pep Guardiola, 53, Kuhusu Mustakabali Wake.
(Telegraph - Usajili Unahitajika)
Galatasaray Wana Nia Ya
Kumsajili Fowadi Wa Ufaransa Anthony Martial Lakini Mchezaji Huyo Mwenye Umri
Wa Miaka 28 Atalazimika Kupunguza Mahitaji Yake Ya Mshahara Baada Ya Kuondoka
Manchester United. (Espn)
Tottenham Wanatazamiwa
Kushindana Na Aston Villa Katika Kinyang'anyiro Cha Kumsajili Kiungo Wa Kati Wa
Chelsea Na Uingereza Conor Gallagher, 24, Ambaye Pia Anasakwa Na Atletico
Madrid Kwa Pauni Milioni 50 . (Mail)
Klabu Ya Besiktas Ya
Uturuki Ilikuwa Kwenye Mazungumzo Na Meneja Wa Zamani Wa Manchester United Ole
Gunnar Solskjaer Kabla Ya Kumteua Meneja Wa Zamani Wa Rangers Giovanni Van
Bronckhorst. (Espn)
Barcelona Wanakaribia
Kumnunua Kiungo Wa Kati Wa Real Sociedad Mhispania Mikel Merino, 27. (Sport -
Kwa Kihispania)