JESHI LA POLISI Mkoa Wa Morogoro
Linamshikilia, Erick Julias (39) Mkazi Wa Mlimba Wilayani Kilombero Kwa Tuhuma
Za Kumuua Na Kumtenganisha Kichwa Pamoja Na Viungo Vingine Mtoto Wake Wa
Kufikia, Johnson Ngonyani (6).
Akizungumza Na Waandishi
Wa Habari Leo Juni 4, 2024, Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Morogoro, Alex Mkama Amesema
Pamoja Na Mtuhumiwa Huyo Kumkata Kichwa, Pia Alimkata Seheme Za Siri (Uume Na
Korodani) Na Viganja Vyote Viwili.
Kamanda Mkama Amesema
Mtuhumiwa Alitenda Ukatili Huo Juni 1 Mwaka Huu Majira Ya Usiku Katika Kitongoji
Cha Kigamboni, Kijiji Cha Mwembeni, Mlimba Wilaya Ya Kilombero.
Amesema Mtuhumiwa Huyo
Amekamatwa Kutokana Na Taarifa Za Raia Wema Na Baada Ya Kuhojiwa Polisi Amekiri
Kufanya Mauaji Hayo Na Ametoa Ushirikiano Kwa Kuonyesha Sehemu Alikoficha
Viungo Hivyo.