MSIMU wa mashindano ya
CAF Interclub 2024/25 utaanza kwa raundi ya awali kati ya tarehe 16 Agosti hadi
18 Agosti, 2024 huku hatua za makundi zikipangwa kufanyika kati ya mwezi Oktoba
hadi mwezi Desemba mwaka 2024.
Klabu ya Yanga itaanza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye raundi ya
pili michuano hiyo na wataanzia ugenini huku Simba Sc ikianzia raundi ya pili
ya kombe la Shirikisho Afrika nayo itaanzia ugenini.
Azam Fc itaanzia raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Coastal Union
wakianzia raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika.
Azam Fc na Coastal Union wataanzia nyumbani kwenye michuano hiyo ambayo inaanza
kurindima kuanzia Agosti 16 mpaka 18.
Tanzania ni miongoni mwa Nchi 12 pekee za Afrika zitakazoingiza timu nne kwenye
mashindano ya CAF. Nchi nyingine ni Algeria, Angola, Ivory Coast, Misri, Libya,
Morocco, Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini, Sudan na Tunisia.
Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya awali utafanyika kati ya
tarehe Julai 1, 2024 hadi Julai 20, 2024.
Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya pili utafanyika kati ya
tarehe Julai 21 hadi Agosti 31, 2024.
Usajili wa wachezaji watakaoshiriki katika hatua ya makundi utafanyika kati ya
Septemba 1 hadi Septemba 30, 2024.
Tags
SPORTS