MKOSOAJI WA KAGAME AZUIWA KUGOMBEA URAIS RWANDA


DIANE RWIGARA, Mkosoaji Mkubwa Wa Rais Kagame Wa Rwanda, Amezuiwa Kugombea Katika Uchaguzi Wa Urais Mwezi Ujao.

Ni Rais Kagame Pekee Na Wanasiasa Wengine Wawili - Frank Habineza Wa Chama Cha Democratic Green Party Na Philippe Mpayimana - Mgombea Huru - Ndio Walioidhinishwa Na Baraza La Uchaguzi.

Bi Rwigara, Ambaye Pia Aliondolewa Katika Uchaguzi Wa 2017, Alitumia X, Ambayo Zamani Ilikuwa Twitter, Kuelezea Kusikitishwa Kwake Na Bw Kagame.

“Kwa Nini Usiniruhusu Kugombea? Hii Ni Mara Ya Pili Unaninyima Haki Yangu Ya Kufanya Kampeni,” Alisema.

Rwigara Mwenye Umri Wa Miaka 42, Ambaye Ni Kiongozi Wa People Salvation Movement (PSM), Awali Aliambia Kipindi Cha Newsday Cha BBC Kwamba Alikuwa Na Matumaini Ya Kuweza Kugombea Wakati Huu.

"Ninawakilisha Idadi Kubwa Ya Wanyarwanda Ambao Wanaishi Kwa Hofu Na Hawaruhusiwi Kuwa Huru Katika Nchi Yao," Alisema.

"Rwanda Inachukuliwa Kuwa Nchi Ambayo Uchumi Umekuwa Ukikua. Lakini Hali Hii Ni Tofauti. Watu Wanakosa Misingi Ya Maisha, Chakula, Maji Na Makazi."

Lakini Ilipotoa Orodha Yake Ya Muda Ya Wagombeaji, Tume Ya Uchaguzi Ilisema Bi Rwigara Alishindwa Kutoa Stakabadhi Sahihi Kuonyesha Kwamba Hakuwa Na Rekodi Ya Uhalifu.

Pia Ilisema Ameshindwa Kuonyesha Kuwa Ana Uungwaji Mkono Wa Kutosha Nchi Nzima Ili Kugombea.

"Kuhusu Mahitaji Ya Uidhinishaji Wa Sahihi 600, Hakutoa Angalau Saini 12 Kutoka Wilaya Nane," Oda Gasinzigwa, Mkuu Wa Tume Ya Uchaguzi, Alinukuliwa Akisema.

Sababu Nyingine Ambayo Tume Hiyo Ilitoa Ni Kwamba Bi Rwigara Alishindwa Kuthibitisha Kwamba Yeye Ni Mnyarwanda Kwa Kuzaliwa.

Aliwahi Kushikilia Uraia Wa Ubelgiji Lakini Akausalimisha Mnamo 2017 Kabla Ya Mara Ya Mwisho Ya Kuwnaia Urais Zabuni .

Lakini Bi Rwigara Ameambia BBC Kwamba Alizaliwa Nchini Rwanda Na Akatupilia Mbali Sababu Nyingine Zote Za Kumzuia Kugombea

Jumla Ya Maombi Tisa Ya Kugombea Urais Yalipokelewa Na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi Ya Rwanda.

Orodha Yao Ya Mwisho Itatangazwa Ijumaa Ijayo Kwani Bado Inazingatia Rufaa Zilizowasilishwa Mapema Katika Mchakato Huo – Ingawaje Muda Umeyoyoma Kwa Kiongozi Huyo Wa PSM Kukata Rufaa.

Mnamo 2017 Alizuiliwa Kufuatia Tuhuma Za Kughushi Saini Za Wafuasi Katika Ombi Lake.

Bi Rwigara Alifungwa Kwa Zaidi Ya Mwaka Mmoja Lakini Akaachiliwa Mwaka Wa 2018 Kwa Tuhuma Za Kuchochea Uasi Na Kughushi. Alisema Mashtaka Hayo Yamechochewa Kisiasa.

Mwezi Machi, Mahakama Ya Rwanda Ilizuia Juhudi Za Kiongozi Mashuhuri Wa Upinzani Victoire Ingabire Kuondoa Marufuku Ya Kugombea Katika Uchaguzi Wa Rais

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT