KATIKA MUENDELEZO Wa
Sherehe Za Maadhimisho Ya Kumbukumbu Ya Miaka 80 Ya D-Day Huko Ufaransa, Rais Wa
Ukraine Volodymyr Zelensky Amekutana Na Wenzake Wa Marekani Joe Biden Na Yule
Wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Biden Aliwasilisha Ujumbe
Huo Kwa Mwenzake Wa Ukraine Volodymyr Zelensky Katika Mkutano Wao Huko Mjini Paris.
Wizara Ya Ulinzi Ya Marekani Imesema Kifurushi Hicho Kinajumuisha Makombora Ya Hawk
Yanayotumiwa Katika Mifumo Ya Ulinzi Wa Anga, Risasi, Makombora Ya Masafa
Marefu Aina Ya HIMARS Na Makombora Ya Kudungua Ndege Aina Ya Stinger. Msaada Huo
Utatumiwa Pia Kukarabati Mifumo Ya Gridi Ya Umeme Ya Taifa Ya Ukraine.
Marekani Ni Mshirika Muhimu
Zaidi Wa Kyiv Na Msambazaji Mkubwa Zaidi Ya Silaha Katika Vita Vyake Dhidi Ya Urusi.
Kulingana Na Wizara Ya Ulinzi Ya Marekani, Washington Imetoa Au Kuahidi Msaada
Wa Kijeshi Kwa Ukraine Wenye Thamani Ya Zaidi Ya Dola Bilioni 51 Tangu Kuanza
Kwa Uvamizi Wa Urusi Februari Mwaka 2022.
Rais Emmanuel Macron Wa Ufaransa
Alimpokea Katika Ikulu Ya Elysée Rais Zelensky Ambaye Baadaye Alipata Pia Fursa
Ya Kulihutubia Bunge La Nchi Hiyo Na Kutoa Wito Kwa Washirika Wake Wa Magharibi
Kuipitia Kyiv Msaada Zaidi Wa Kijeshi Huku Akipongeza Hatua Ya Ufaransa Kuamua
Kuipatia Ukraine Ndege Za Kivita Chapa Mirage-2000.
Rais Zelensky Amewaambia
Wabunge Wa Ufaransa Kuwa Iwapo Putin Hatozuiwa, Hatokomea Ukraine Na Ataendelea
Na Uvamizi Wake Hadi Kwenye Mataifa Mengine Ya Magharibi. Zelensky Ameshukuru
Kwa Misaada Na Akasema Kama Ilivyokuwa Miaka 80 Iliyopita, Ukatili Wa Putin Kamwe Hautakiwi Kushinda. Aidha Zelensky Amewashukuru
Washirika Wake Wa Magharibi Na Kusisitiza Kuwa Bado Safari Ni Ndefu:
"Ninashukuru Kwa
Yote Mnayoyafanya, Na Kwa Hahika Ni Mengi Mno. Lakini Ili Kufikiwa Amani Ya
Haki, Kuna Mambo Zaidi Ambayo Ni Lazima Yafanyike. Na Hii Wala Si Lawama, Ni
Ukumbusho Tu Wa Jinsi Ya Kuushinda Uovu. Tunahitaji Kufanya Zaidi Leo Kuliko
Tulivyofanya Jana, Na Hivyo Huko Mbeleni Kuliko Wakati Wowote, Tunaweza
Kukaribia Zaidi Amani."
Maadhimisho Ya Kumbukumbu
Ya Miaka 80 Ya D-Daymaadhimisho Ya Kumbukumbu Ya Miaka 80 Ya D-Day
Maadhimisho Ya Kumbukumbu
Ya Miaka 80 Tangu Vikosi Washirika Vikiongozwa Na Marekani Na Uingereza Vilipotuwa
Katika Fukwe Za Normandy, Ufaransapicha: Gareth Fuller/AP/Picture Alliance
Maadhimisho Haya Ya
Kumbukumbu Ya Miaka 80 Tangu Vikosi Washirika Vikiongozwa Na Marekani Na Uingereza
Vilipotuwa Katika Fukwe Za Normandynchini Ufaransa, Ili Kuanza Operesheni Ya
Kijeshi Ya Kulikomboa Eneo Kubwa La Kaskazini Na Magharibi Mwa Ulaya Dhidi Ya
Wanazi Wa Ujerumani Wakati Wa Vita Vya
Pili Vya Dunia. Licha Ya Askari Karibu 150,000 Kuwasili Normandy Juni 6 Mwaka
1944, Vita Hivyo Vya Pili Vya Dunia Viliendelea Hadi Mei Mwaka 1945.
Licha Ya Kuwa Maadhimisho
Haya Yanakumbushia Historia Mbaya Ya Ujerumani, Kansela Olaf Scholz Alikumbusha
Tu Kwamba D-Day Haikuwa Na Manufaa Kwa Ufaransa Na Washirika Wengine Wa Ulaya Wakati
Huo, Bali Pia Ilikuwa Siku Ya Ukombozi Kwa Ujerumani Kwa Kuwa Ilijenga Msingi
Wa Uhuru Na Demokrasia.