ALIYEKUWA
DIWANI Wa Kata Ya Kamena Halmashauri Ya Wilaya Ya Geita Mkoani Geita, Peter
Kulwa (67) Mkazi Wa Kata Ya Kamena Aliyefariki Juni 13, 2024 Wakati Alipokuwa
Akipatiwa Matibabu Katika Hospitali Ya Kamanga Mkoani Mwanza Amezikwa Leo
Nyumbani Kwake Huku Akiacha Watoto 34 Wajukuu 129 Na Vitukuu 10.
Akisoma
Historia Ya Marehemu Mjukuu Wa Diwani Hiyo Anayefahamika Kwa Jina La Makutano
Sadiki Amesema Babu Yao Alikuwa Akisumbuliwa Na Ugonjwa Wa Kisukari Ambao
Alikuwa Akizunguka Nao Kwa Kutafta Huduma Ya Matibabu Ambapo Alikuwa Akipatiwa
Matibabu Katika Hospitali Ya Kamanga Jijini Mwanza Alikokutwa Na Umauti.
"
Ugonjwa Ulimuanza Mwezi Mei 2002 Na Alipekelekwa Hospitali Mbalimbali Ikiwemo
Ya Geita, Singida Pamoja Kamanga Hadi Kufikia 2023 Ambapo Alipata Nafuu
Ilipofika Tarehe 10/4 /2024 Hali Yake Ilibadilika Ghafla Alikimbizwa Hospital
Kamanga Na Kufika Tarehe 13/6/2024 Majira Ya Saa Tisa Alasiri Alifariki Dunia ,
" Mjukuu Wa Marehemu Sadick.
Viongozi
Wa Chama Na Serikali Wamehudhuria Mazishi Ya Kiongozi Huyo Akiwemo Mwenyekiti
Wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Geita , Nicholaus Kasendamila , Mkuu Wa Wilaya
Ya Geita , Hashim Komba , Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Geita ,
Barnabas Mapande , Wakuu Wa Idara Kutoka Katika Halmashauri Hiyo Pamoja Na
Wananchi.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI