UMOJA
Wa Mataifa Umeongeza Jeshi La Israel, Hamas Na Tawi La Kijeshi La Palestina
Islamic Jihad Kwa Mara Ya Kwanza Kwenye Orodha Yake Ya Wahalifu Kwa Kukiuka
Haki Za Watoto.
Vitengo
Hivyo Vitatu, Pamoja Na Pande Zinazopigana Nchini Sudan, Vimeoredheshwa Kwa
Mauaji Na Ulemavu Wa Watoto.
"Watoto Waliuawa Na Kulemazwa Kwa Idadi Isiyo Na Kifani", Ripoti Ya Children In Armed Conflict Ilisema.
Katibu
Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa António Guterres Alisema Mzozo Kati Ya Israel Na
Makundi Ya Wapalestina Umesababisha Ukiukwaji Mkubwa Kwa Kiwango Ambacho
Hakijawahi Kushuhudiwa, Haswa Huko Gaza.
"Watoto
Walibeba Mzigo Mkubwa Wa Migogoro Ambayo Ilikuwa Na Malalamishi Ya
Kutozingatiwa Kabisa Kwa Haki Za Mtoto, Haswa Haki Ya Asili Ya Kuishi,"
Ripoti Hiyo Ilisema.
Ripoti
Hiyo Ilisema Mzozo Wa Gaza Umesababisha Ongezeko La 155% La Kile Ilichokitaja
Kama "Ukiukwaji Mkubwa" Dhidi Ya Watoto.
Umoja
Wa Mataifa Ulithibitisha Zaidi Ya Ukiukwaji Mkubwa Wa Visa 8,000 Dhidi Ya
Watoto 4,247 Wa Kipalestina Na Watoto 113 Wa Israeli Mnamo 2023, Ripoti Hiyo
Ilisema.
Lakini
Uhakiki Unaendelea Huku Maelfu Ya Ripoti Kuhusu Watoto Waliofariki Na
Kujeruhiwa Bado Zikihitaji Kuangaliwa.
"Matukio
Mengi Yalisababishwa Na Matumizi Ya Silaha Za Milipuko Katika Maeneo Yenye Watu
Wengi Na Vikosi Vya Usalama Vya Israeli," Ripoti Hiyo Inasema.
Mjumbe
Wa Israel Katika Umoja Wa Mataifa Gilad Erdan Alisema Wiki Iliyopita Aliarifiwa
Kuwa Jeshi La Israel Limeongezwa Kwenye Orodha Hiyo, Akisema "Ameshtushwa
Na Kuchukizwa Na Uamuzi Huo Wa Aibu".
Hamas
Na Palestina Islamic Jihad Pia Ziliwekwa Kwenye Orodha Ya Mauaji, Kujeruhi Na
Kuwateka Nyara Watoto.
Makundi
Hayo Mawili - Ambayo Yameteuliwa Kama Mashirika Ya Kigaidi Na Israel, Uingereza
Na Nchi Zingine - Bado Hayajatoa Maoni Juu Ya Ripoti Hiyo.
Israel
Ilianza Mashambulizi Yake Baada Ya Hamas Kushambulia Jamii Karibu Na Gaza Tarehe
7 Oktoba Mwaka Jana, Na Kuua Takriban Watu 1,200 Wakiwemo Watoto 38 Na Kuchukua
Mateka 251 Wakiwemo Watoto 42, Kulingana Na Baraza La Kitaifa La Mtoto La Israel.
Wizara
Ya Afya Inayoendeshwa Na Hamas Huko Gaza Imesema Watu 36,731 Wameuawa Na Israel
Kutokana Na Mashambulizi Ya Mabomu Na Ardhini.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI