UKANDA WA GAZA Umeendelea
Kushambuliwa Jumamosi Hii Huku Waziri Wa Israel Anayehusika Na Vita Akitishia
Kujiuzulu.
Serikali Ya Israel Inakabiliwa
Na Shinikizo Kubwa Kutokana Na Mwenendo Wake Katika Operesheni Ya Kijeshi Huko Gaza.
Kwa Mujibu Wa Mashuhuda
Na Ripoti Za Waandishi Wa Habari Wa Shirika La Habari La AFP, Mashambulizi Ya Israel
Yalihanikiza Maeneo Tofauti Ya Ukanda Wa Gaza Na Kuelekezwa Zaidi Upande Wa
Katikati Mwa Eneo Hilo La Palestina.
Mashambulizi Hayo
Yanajiri, Licha Ya Uchunguzi Dhidi Ya Israel Baada Ya Ndege Zake Za Kivita
Kufanya Shambulizi Kwenye Shule Inayosimamiwa Na Shirika La Umoja Wa Mataifa Linalowahudumia
Wakimbizi Wa Kipalestina UNRWA.
Jeshi La Israel Lilikiri
Kufanya Shambulio Hilo Katika Kambi Ya Wakimbizi Ya Nuseirat, Likidai Kuwa
Lililenga Kambi Ya Wanamgambo Wa Hamas Na Kuwaua Magaidi 17.