SAUDI ARABIA Inalenga
Kupokea Wageni Mahujaji Wa Kiislamu Zaidi Ya Milioni Mbili Wakati Wa Hija Ya
Mwaka Huu.
Kwa Mara Ya Kwanza, Saudi
Arabia Itatumia Mchanganyiko Wa Lami Na Mpira Kwa Ajili Ya Watembea Kwa Miguu
Ili Kuwakinga Na Joto Kali Linalokabili Eneo Hilo.
Siku Ya Alhamisi, Waziri Wa
Huduma Za Uchukuzi Wa Saudi Arabia, Saleh Bin Nasser Al-Jasser, Alitangaza Kuwa
Jumla Ya Teknolojia Mpya 32 Zitafanyiwa Majaribio Wakati Wa Msimu Wa Hija Ili
Kukidhi Mahitaji Ya Kila Siku Wakati Wa Hija Hiyo.
Al-Jasser Aliweka Wazi
Kuwa Teknolojia Hizo Zitatumika Kwa Mara Ya Kwanza Kwenye Barabara, Hususani
Mchanganyiko Wa Lami Na Mpira Kwa Ajili Ya Njia Ya Watembea Kwa Miguu Wakiwemo
Mahujaji.
Vile Vile Amedokeza Kuwa
Kutandazwa Tabaka Jeupe Kutasaidia Kupunguza Joto Kwa Zaidi Ya Nyuzi Joto 15,
Likiwemo Eneo Linalopakana Na Msikiti Wa Namira Huko Arafat, Pamoja Na
Kuongezeka Kwa Matumizi Ya Ndege Zisizo Na Rubani Kukagua Na Kutathmini Mtandao
Wa Barabara.
Waziri Huyo Ameongeza
Kuwa Mfumo Wa Usafiri Wa Nchi Hiyo Umejipanga Kikamilifu Kuhakikisha Mahujaji
Wanasafirishwa Salama Kupitia Njia Mbalimbali Za Anga, Nchi Kavu, Baharini Na
Reli, Toka Wanapowasili Saudi Arabia Kwa Ajili Ya Ibada Ya Hija Na Kuhakikisha
Pia Wanaondoka Salama.
‘Viwanja Sita Vya Ndege
Katika Ufalme Vimeanzishwa Ili Kupokea Ndege Za Mahujaji, Vikipanga Safari Za
Ndege 7,700 Na Kutoa Viti Milioni 3.4 Ndani Ya Ndege,” Alisema.