KISA CHA MAAMBUKIZI YA MAFUA YA NDEGE CHAGUNDULIKA INDIA


SHIRIKA La Afya Duniani WHO Limegundua Kisa Cha Maambukizi Ya Homa Ya Mafua Ya Ndege Kwa Mtoto Wa Miaka Minne Inayosababishwa Na Virusi Aina Ya H9N2 Huko Katika Jimbo La West Bengal Nchini India.

Mgonjwa Alilazwa Katika Chumba Cha Wagonjwa Mahututi Kutokana Na Hali Mbaya Iliyomkabili Katika Mfumo Wake Wa Upumuaji, Homa Kali Na Maumivu Ya Tumbo Mwezi Februari, Na Aliruhusiwa Miezi Mitatu Baadae Baada Ya Kupata Matibabu.

Inaelezwa Mgonjwa Huyo Alitokea Katika Mazingira Ambayo Yanafugwa Kuku Nyumbani Kwao Na Hapakuwa Na Mtu Anayejulikana Aliyeripoti Dalili Za Ugonjwa Wa Kupumua Kati Ya Familia Yake Na Mawasiliano Mengine.WHO Iliongeza Kwa Kusema Taarifa Juu Ya Hali Ya Chanjo Na Maelezo Ya Matibabu Ya Kukabiliana Na Virusi Hayakupatikana Wakati Mgonjwa Alipowasilishwa Hospitali.

Haya Ni Maambukizi Ya Pili Ya Binadamu Ya Mafua Ya Ndege Ya Virusi Aina Ya H9N2 Kutoka India, Ya Kwanza Yalitokea  2019.

JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI

BONYEZA HAPA KUJISAJIRI



Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT