Hapo Awali Maporomoko Ya Maji
Yapatikanayo Mlima Yuntai Nchini China Yalitambulika Kuwa Ni Ya Asili (Natural)
Siyo Ya Kutengeneza (Artificial), Yana Urefu Wa Futi 1024, Yanadaiwa Kuwa Maporomoko
Ya Maji Marefu Zaidi Nchini China, Huku Kila Mwaka Yakivutia Watalii Wengi
Kutoka Ndani Na Nje Ya China.
Mwaka 2019 Zaidi Ya Watu
Milioni 11 Walienda Mlima Yuntai Kwa Ajili Ya Kutalii Kwenye Hayo Maporomoko Ya
Maji.
Hivi Karibuni Watalii Watembeao
Kwa Miguu (Hakers) Wamegundua Kuwa Chanzo Cha Maporomoko Hayo Ya Maji Siyo
Asilia Bali Kimetengengezewa, Juu Kabisa Ya Maporomoko Ya Maji Wamekuta Bomba
La Maji.
Baada Ya Sakata Hilo Viongozi
Wa Mamlaka Inayohusika Kusimamia Eneo Hilo Wamedai Kuwa Maporomoko Hayo Ya Maji
Ni Asilia Kabisa Ila Kipindi Cha Kiangazi Huwa Maji Yanapungua Hivyo Wamefanya
Maboresho Kadhaa Ili Kuongeza Mvuto Zaidi Pia Chanzo Kisikauke Maji.
“The Yuntai Mountain Waterfall
Is A Natural Landscape Feature. But, As A Seasonal Attraction, In Order To
Ensure That Tourists Do Not Go Away Disappointed, We Made A Small Enhancement
During The Dry Season.”----Msemaji Wa Kivutio Hicho.
Watu Wengi Mitandaoni Wanadai Kwamba Maporomoko Hayo Ya Maji Hayastahili Kupewa Sifa Na Kuheshimiwa Kama Hapo Awali Maana Tayari Imegundulika Siyo Asilia Lakini Wengine Wanadai Tu Yaendelee Kupewa Sifa Na Kuheshimiwa Kwani Chanzo Cha Maji Kuwa Asilia Au Cha Kutengenezwa Hakipunguzi Chochote Kwenye Muonekano Wa Maporomoko Hayo Ya Maji.