DAVID KAFULILA, Mkurugenzi
Wa Ubia Kati Ya Sekta Ya Umma Na Sekta Binafsi (PPP) Kupitia Ukurasa Wake Wa
Mtandao Wa Kijamii Wa X, Amechambua Kwamba Kukopa Kwa Ajili Ya Miradi Ya
Maendeleo Ndiyo Njia Ya Kujenga Uchumi.
Ameeleza Kuwa Nchi Zote
Kubwa Duniani Zinajengwa Kwa Mikopo Ndiyo Sababu Wakati Uchumi Wa Dunia
Umefikia USD Trilioni 105, Deni Lote La Dunia (Serikali Na Binafsi).
Deni La Serikali Zote
Limefikia USD Trilioni 97, Sawa Na 97% Ya Uchumi Wa Dunia Na Deni Lote La Dunia
Kwa Jumla Ni USD 315... Zaidi Ya 300% Ya GDP Ya Dunia.
Vietnam Ni Nchi Ya Mfano
Duniani Kwa Muujiza Wa Kukuza Uchumi Ndani Ya Muda Mfupi, Kwani Mwaka 1990,
Uchumi Wa Vietnam Ulikuwa USD Bilioni 6.4, Mbele Kidogo Ya Tanzania Iliyokuwa
Na USD Bilioni 4.5 Na Nyuma Ya Kenya Iliyokuwa Na USD Bilioni 8.4, Lakini Miaka
30 Baadaye, Uchumi Wa Vietnam Ni USD Bilioni 400, Karibu Mara 4 Ya Kenya Na
Mara 5 Ya Tanzania.
Hata Hivyo, Mwaka 2007,
Wakati Uchumi Wa Vietnam Ukiwa USD Bilioni 77, Sawa Na Tanzania Leo, Uwiano Wa
Deni Kwa Uchumi Ulikuwa Asilimia 43% Karibu Sawa Na Uwiano Wa Deni Kwa Uchumi
Wetu Tanzania.
Kukopa Kujenga Uchumi
Ndiyo Njia!