MAREKANI
Imetangaza Msaada Mwingine Wa Dola Milioni 315 Kwa Ajili Ya Kuwasaidia Raia Wa Sudan
Wanaokabiliwa Na Njaa Kutokana Na Vita Vya Wenyewe Wa Wenyewe Vilivyopindukia
Mwaka Mmoja.
Msaada
Huo Utajumuisha Chakula Na Maji Ya Kunywa Pamoja Na Kutoa Huduma Za Matibabu
Ikiwemo Uchunguzi Na Tiba Kwa Watoto Walio Na Utapiamlo.
Umetolewa
Katika Wakati Makadirio Yanaonesha Kiasi Watu Milioni 5 Ndani Ya Sudan Wanakabiliwa
Na Njaa Kali Na Chakula Pia Hakipatikani Kwenye Mataifa Jirani Ambako Raia
Milioni 2 Wa Sudan Wamekimbilia Kuepuka Mapigano.
Tangazo
La Msaada Huo Wa Marekani Limeambatana Na Wito Wa Serikali Mjini Washington Wa
Kuzirai Pande Hasimu Kukomesha Tabia Ya Kuzuia Usambazaji Wa Mahitaji Ya Kiutu
Kwa Raia.
Mashirika
Ya Misaada Ya Kimataifa Ikiwemo Lile La Marekani, USAID Yametoa Hadhari Kwamba Sudan
Inaelekea Pabaya Na Ukosefu Wa Chakula Unaweza Kuzusha Baa La Njaa Kushinda
Lile Lililoikumba Ethiopia Mwanzoni Mwa Miaka 1980.
Licha
Ya Miito Ya Kimataifa Pande Hasimu Ambazo Ni Jeshi La Nchi Hiyo Na Kikosi Cha
Wanamgambo Wa RSF Bado Wanapambana Kuwania Madaraka.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI