RAIS
WA AFRIKA KUSINI Cyril Ramaphosa Amechaguliwa Na Wabunge Wa Nchi Hiyo Kuanza
Muhula Wa Pili Madarakani.
Uchaguzi
Huo Wa Rais Unafuatia Chama Cha Ramaphosa Cha African National Congress, ANC,
Kupata Makubaliano Na Vyama Vingine Kuunda Serikali Ya Umoja Wa Kitaifa.
Ramaphosa
Amechaguliwa Kwa Wingi Mkubwa Wa Kura Katika Kikao Cha Kwanza Cha Bunge Jipya
La Nchi Hilo Kilichofanyika Jana Mjini Cape Town, Kiasi Wiki Mbili Baada Ya
Kufanyika Uchaguzi.
Amepata
Kura 283 Dhidi Ya Mwanasiasa Machachari Julius Malema Anayeongoza Chama Cha
Mrengo Mkali Wa Kushoto Cha Economic Freedom Fighters Aliyeambulia Kura 44.
Ramaphosa
Mwenye Umri Wa Miaka 71 Amepata Ushindi Huo Kwa Kuungwa Mkono Na Chama Cha Pili
Kwa Ukubwa Nchini Humo Cha Democratic Alliance Na Vyama Vingine Vidogo.
Vyama
Hivyo Vilifikia Makubaliano Ya Kuunda Seriali Ya Pamoja Na ANC Kufuatia Chama
Hicho Tawala Kukosa Wingi Wa Viti Bungeni Katika Uchaguzi Wa Mei 29.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI