SAA
CHACHE Baada Ya Aliyekuwa Mwenyekiti Wa Bodi Ya Simba Salim Mhene 'Try Again'
Kujiuzulu Nafasi Hiyo, Mwekezaji Za Klabu Hiyo Mohammed Dewji 'Mo' Ameibuka Na
Mambo Sita Huku Akitangaza Kurejea Kwenye Nafasi Hiyo.
Mapema
Leo Jioni, Try Again Alitangaza Rasmi Kujiuzulu Nafasi Hiyo, Kufuatia
Changamoto Zilizoikumba Klabu Hiyo Ikianguka Kwa Matokeo Kwa Kushika Nafasi Ya
Tatu Kwenye Msimu Uliomalizika.
Akitangaza
Muda Mfupi Uliopita Mo Ameridhia Kurejea Kwenye Kuongoza Bodi Ya Klabu Hiyo
Kuhakikisha Anarejesha Utulivu Ambao Ulipotea Ndani Ya Miaka Mitatu.
Katiika
Taarifa Yake Kwa Wanasimba Mo Ameyataja Mambo Sita Yaliyoikwamisha Simba
Yakiwemo Mvurugano Na Makundi Yaliyozalishwa Na Uchaguzi Wa Viongozi Wa Juu Kwa
Upande Wa Wanachama.
"Tangu
Uchaguzi Upite Tumekuwa Na Mvurugano Na Makundi Yaliyotokana Na Uchaguzi, Hili
Limesababisha Migongano Mbalimbali Ndani Ya Klabu Yetu, Niwaombe Wanasimba
Wenzangu Tuvunje Makundi Na Turudi Kushirikiana Kama Kauli Yetu Inayosema Simba
Nguvu Moja,"Amesema Mo.
Ameelezea Pia Namna Mabadiliko Ya Benchi La Ufundi Na Eneo Hilo Kutokuwa Imara Limechangia Kuirudisha Nyuma Timu Hiyo Kongwe.
"Tulipoteza
Ubora Wa Kucheza Mpira Wetu Wa 'Pira Biriani' Kutokana Na Mabadiliko Ya
Makocha, Nitashirikiana Na Viongozi Wenzangu Kuunda Benchi Imara La Ufundi
Litakaloturudishia Ubora Wetu."
Tajiri
Huyo Ameutaja Pia Usajili Usiokidhi Kiu Ya
Wanasimba Ukichangia Kuirudisha Nyuma Timu Hiyo Kutawala Kwa Kuchukua
Vikombe Vya Ndani Ya Nchi.
"Tumekuwa
Tukisajili Wachezaji Wengi Ambao Wameshindwa Kukidhi Kiu Ya Wanasimba, Nataka
Niwaambie Wanasimba Tutakwenda Kufanya Usajili Mzuri Utakaorudisha Ubora Wa
Kikosi Chetu."
Ameelezea
Pia Kitokamilika Kwa Mchakato Wa Mabadiliko Ya Mfumo Wa Uendeshaji Na Kwamba
Wanakwenda Kuhakikisha Hatua Zilizosalia Zinamalizika Sambamba Na Kuboresha
Miundo Mbinu Ya Viwanja Vyao Ya Mazoezi Vilivyopo Bunju Ambapo Amekiri Kuwa
Havikidhi Vigezo.
"Tutakwenda
Kumalizia Mchakato Wa Mabadiliko Ili Kila Mwanachama Aweze Kumiliki Hisa Zake,
Suala La Tano Ni Miundo Mbinu Yetu Ya Eneo La Viwanja Nayo Tutaiboresha Ili
Iendane Na Hadhi Ya Simba.
Mo
Amemalizia Kwa Kutaja Eneo La Uwekezaji Kwa Soka La Vijana Na Kwamba Wataweka
Nguvu Kubwa Itakayozalisha Vipaji Kwa Kuanzia Chini.
Huku
Akisema Kuwa Ameongea Na Try Again Na Amekubali Kubaki Kama Mjumbe Wa Bodi
Upande Wa Mwekezaji.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI