RAIS VALDIMIR PUTIN Ameonya
Jana Jumatano Kwamba Urusi Inaweza Ikawapatia Mataifa Mengine Makombora Ya
Masafa Marefu Kwa Ajili Ya Kushambulia Maeneo Lengwa Kwenye Mataifa Ya
Magharibi.
Hatua Hii Amesema Itakuwa
Ni Jibu Ya Ruhusa Iliyotolewa Na Washirika Wa Jumuiya Ya NATO Kwa Ukraine Kutumia
Silaha Inazopewa Na Magharibi Kuishambulia Urusi.
Putin Aidha Amethibitisha
Kwa Mara Nyingine Kuhusu Utayari Wa Kutumia Silaha Za Nyuklia Ikiwa Kutakuwa Na
Kitisho Chochote Kwenye Eneo Lake.
Amesema Hatua Hiyo Ya
Magharibi Itazidi Kudhoofisha Usalama Wa Kimataifa Na Kuchochea Matatizo
Makubwa, Na Kuashiria Wazi Ushiriki Wake Wa Moja Kwa Moja Kwenye Vita Kati Ya Urusi
Na Ukraine Na Kuongeza Kuwa Wana Haki Ya Kuchukua Hatua Kama Hiyo.
Putin Alikuwa Akizungumza
Na Waandishi Wa Habari Wa Vyombo Vya Magharibi, Jambo Ambalo Analifanya Kwa
Nadra Mno Tangu Alipoivamia Ukraine.
Marekani Na Ujerumanihivi
Karibuni Waliiruhusu Ukraine Kutumia Makombora Ya Masafa Marefu Waliyoipatia
Kushambulia Baadhi Ya Maeneo Ndani Ya Urusi.
Siku Ya Jumatano, Afisa
Mmoja Wa Magharibi Pamoja Na Seneta Wa Marekani Walisema Ukraine Imetumia
Silaha Walizopewa Na Taifa Hilo Kushambulia Ndani Ya Urusi Chini Ya Idhini Hiyo
Inayosimamiwa Na Rais Joe Biden, Ambapo Ukraine Watatumia Silaha Hizo, Lakini
Kwa Masharti, Katika Kuupigania Mji Wake Wa Kharkiv.
Putin Asisitiza Kwamba Urusi
Haikuanzisha Vita Nchini Ukraine
"Kama Mtu Anadhani
Inawezekana Kupeleka Silaha Kwenye Uwanja Wa Vita Ili Kushambulia Eneo Letu Na
Kutuletea Matatizo, Kwa Nini Na Sisi Hatuna Haki Ya Kupeleka Silaha Kama Hizo
Kwenye Maeneo Mengine Duniani Ambako Wanaweza Kushambulia Maeneo Muhimu Kwenye
Mataifa Ya Magharibi?" Alihoji Putin.
"Hilo Litakuwa Jibu
Linalowiana. Tutafikiria Kuhusu Hilo," Aliwaambia Waandishi Hao Wa Habari,
Huku Akipuuzilia Mbali Madai Kwamba Urusi Inapanga Kuwashambulia Wanachama Wa NATO.
Putin, Ametumia Pia Fursa
Hiyo Kurudia Na Kusisitiza Kwamba Nchi Yake Haikuanzisha Vita Dhidi Ya Ukraine,
Na Badala Yake Alipeleka Lawama Zake Kwenye Vuguvugu Lililoanza Mnamo Mwaka
2014 La Wanaounga Mkono Mataifa Ya Magharibi
"Kila Mmoja Anadhani
Urusi Ilianzisha Vita Nchini Ukraine. Ningependa Kusisitiza Kwamba Si Magharibi
Wala Ulaya Anayetaka Kukumbuka Namna Janga Hili Lilivyoanza," Alisema Putin.
Hata Hivyo, Putin Alikataa
Kutaja Idadi Ya Wanajeshi Waliokufa Kwenye Vita Hivyo Vya Miaka Miwili, Akisema
Tu Kwamba Idadi Ya Vifo Vya Wanajeshi Wa Ukraine Imezidi Mara Tano Ya Wale Wa Urusi.