MBEYA. “Nilisikia
Kitu Kizito Kikiniangukia.” Ni Kauli Ya Mmoja Wa Majeruhi, James Mwasa Mkazi Wa
Nzovwe, Jijini Mbeya Akisumulia Jinsi Ajali Hiyo Ilivyotokea Na Kusababisha
Vifo Vya Watu 13 Papo Hapo Na Wengine 18 Kujeruhiwa Ikihusisha Magari Matatu,
Bajaji, Pikipiki Na Guta Jijini Mbeya.
Ajali Hiyo Imetokea
Leo Jumatano Juni 5, 2024 Katika Mteremko Wa Simike, Eneo La Mbembela Likihusisha
Lori Linalodaiwa Kufeli Breki Na Kwenda Kuyagonga Magari Mengine Mawili Kabla
Ya Kuifikia Pikipili, Bajaji Na Guta.
Majeruhi Wa Ajali Hiyo
Wamelazwa Katika Hospitali Ya Kanda, Mbeya Kwa Matibabu Zaidi, Huku Wanane
Wakiwa Wamewekwa Kwenye Chumba Cha Uangalizi Maalumu (ICU).
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa
Mbeya, Benjamini Kuzaga Ameiambia Mwananchi Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni
Dereva Wa Lori Ambaye Alishindwa Kulimudu Baada Ya Kufeli Breki.
Amesema Dereva Wa Gari
Hilo Anashikiliwa Na Polisi Kutokana Na Ajali Hiyo.
“Gari Hilo Aina Ya Scania
Lilikuwa Likitokea Mbeya Kuelekea Tunduma Lilikosa Uelekeo Kutokana Na Kufeli
Breki Na Likaligonga Gari Dogo Aina Ya Toyota Harrier, Kisha Kuigonga Coaster Ya
Abiria Iliyokuwa Ikitokea Tunduma Kuelekea Mbeya Mjini Na Kusababisha Vifo 13
Na Majeruhi 18,” Amesema Kamanda Huyo.
Amesema Mpaka Sasa Bado
Hawajajua Wapi Walipo Madereva Wa Pikipiki, Bajaj Na Guta, Kama Ni Miongoni Mwa
Majeruhi Au Waliofariki Dunia.
Amesema Baadhi Ya Majeruhi
Hali Zao Si Nzuri Na Jeshi La Polisi Litaendelea Kutoa Taarifa Zaidi Kadiri
Zitakvyowafikia Kuhusiana Na Hali Za Majeruhi Hao.
Akizungumzia Eneo
Ilipotokea Ajali, Kamanda Kuzaga Amesema Ni Korofi Na Mara Zote Askari Wa
Usalama Barabarani Hutoa Tahadhari Kwa Madereva Kuwa Makini Wanapolifikia Eneo
Hilo Pamoja Na La Mlima Shamwengo.
“Zipo Hatua Tunachukua
Kwa Madereva, Ikiwamo Kuwapatia Elimu, Lakini Hapa Ni Eneo Lenye Mteremko Mkali
Na Kuna Ujenzi Wa Barabara Wa Njia Nne Unaendelea, Ukikamilika Huenda
Ajali Kama Hizi Zinazokatisha Uhai Wa Watu Wengi Kwa Wakati Mmoja Zitapungua
Kwa Kiwango Kikubwa,” Amesema Kamanda Huyo.