RAIS VLADIMIR PUTIN amesema
Urusi inasalia mshirika muhimu wa kibiashara ulimwenguni licha ya kuelemewa na
ongezeko la vikwazo vya magharibi.
Putin amesema hayo jana
Ijumaa kwenye Jukwaa la 27 la Kimataifa la Uchumi, SPIEF, mjini St. Petesburg
na kuongeza kuwa Urusi ni miongoni mwa mataifa vinara kiuchumi, mbele ya
Ujerumani akiangazia takwimu zinazozingatia uwezo wa manunuzi.
Kwenye hotuba mbele ya
mamia ya wahudhuriaji, Putin alitoa wito wa kutanua ushirikiano katika masuala
ya teknolojia na kutangaza matarajio yenye lengo la kuvutia wawekezaji zaidi
kutoka nje.
Mataifa ya magharibi
yameiwekea Urusi msururu wa vikwazo baada ya kuivamia Ukraine miaka miwili
iliyopita.
Tangu kuwekwa kwa vizuizi
hivyo vya kibiashara, Urusi imegeukia washirika wapya na hususan China, lakini
pia India, Afrika na Amerika ya Kusini.