RAIS EMMANUEL MACRON Amesema
Ufaransa Inapanga Kuanza Mara Moja Kuwafunza Marubani Na Mafundi Wa Ukraine Namna
Ya Kuziendesha Ndege Za Kivita Aina Ya Mirage, Ambazo Imeahidi Kuzipeleka Kyiv.
Macron Amesema Hayo Baada
Ya Mazungumzo Na Rais Wa Ukraine Volodymyr Zelensky Katika Makazi Ya Rais Ya Élysée
Jijini Paris.
Macron Hata Hivyo Bado
Hajaainisha Idadi Ya Ndege Ambazo Ufaransa Na Mataifa Mengine Wanataraji
Kuzipeleka Ukraine Ambayo Inapambana Na Urusi.
Ufaransa Bado Inahitaji
Kuhitimisha Mchakato Huo Kwa Kuamua Juu Ya Idadi Ya Ndege Itakayopeleka Pamoja
Na Mazungumzo Ya Mpango Wa Pamoja Ulioanza Miezi Kadhaa Iliyopita Na Mataifa
Washirika.
Rais Volodymyr Zelensky Amemshukuru
Macron Kwa Ahadi Hiyo Ya Kupeka Ndege Hizo Za Kijeshi Za Mirage Ili Kusaidia
Juhudi Za Kyiv Za Kulinda Anga Zake Dhidi Ya Mashambulizi Ya Urusi.
Ukraine Yaishukuru Ulaya,
Katikati Ya Hofu Dhidi Ya Mashambulizi Makali Ya Urusi
"Ndege Zenu,
Mheshimiwa.. Ndege Za Kivita, Zinazoendeshwa Na Marubani Wa Ukraine Zinadhihirisha
Uthabiti Wa Ulaya, Kwamba Ulaya Ni Thabiti Kuliko Uovu," Alisema Zelensky Siku
Ya Ijumaa Katika Hotuba Yake Kwenye Bunge La Ufaransa, Mjini Paris.
"Ufaransa Inapanga
Kuanza Mara Moja Kuwafundisha Marubani Na Mafundi Kuhusiana Na Uendeshwaji Wa
Ndege Hizo. Hili Litaanza Hapa Ufaransa Katika Siku Chache Zijazo,"
Alisema Macron Katika Kasri La Rais La Élysée.
Macron Alitangaza Pia
Msaada Wa Dola Milioni 200 Kwa Ajili Ya Kuisaidia Ukraine Kiuchumi Na Hususan
Makampuni, Yanayotaka Kuwekeza Kwenye Miundombinu Iliyoharibiwa Vibaya Na
Mashambulizi.
Zelensky Aidha Amewaambia
Wabunge Wa Ufaransa Mapema Siku Ya Ijumaa Kwamba Rais Wa Urusi Vladimir Putin Ni
"Mpinzani Wa Ulaya" Na Hataumaliza Uvamizi Wake Nchini Ukraine,
Akiifananisha Kampeni Ya Moscow Na Ile Ya Adolf Hitler Wakati Wa Vita Vya Pili Vya
Dunia.
"Mazingira Yanafanana
Na Ya Sasa, Kama Ya Miaka Ya 1930, Wakati Hitler Alipokuwa Akifanya Hivihivi
Dhidi Ya Majirani Yake," Alisema Zelensky.