KIWANGO Cha Uzazi Nchini
Japan Ambacho Kimezidi Kushuka Kwa Kasi Kwa Miaka Mingi Na Kufikia Rekodi
Nyingine Ya Chini Zaidi Hivi Karibuni, Kimeifanya Serikali Ya Nchi Hiyo
Kuongeza Ubunifu Kwenye Kampeni Zake Za Kuwahimiza Vijana Kuoa Na Kuanzisha
Familia Ambapo Sasa Imezindua App Ya Simu Ambayo Kazi Yake Mahususi Ni
Kurahisisha Watu Kuchumbiana.
Kwenye App Hiyo Na Tovuti
Yake, Watumiaji Lazima Wawe ‘Single’ Wakiwa Na Umri Zaidi Ya Miaka 18 Na Wawe
Wenye Hamu Ya Kuoa Na Kuolewa Pia Wawe Wanaishi Au Kufanya Kazi Katika Jiji La
Tokyo Ambapo Watumiaji Wataombwa Kuweka Sifa Ambazo Wanatamani Kuzikuta Kwa Wenza
Wao Wa Maisha.
Ndani Ya App Hiyo Yenye
Mambo Mbalimbali, Pia Inaorodhesha Hatua Nyingine Za Serikali Kusaidia Wanandoa
Kama Vile Kutoa Taarifa Kuhusu Ku-Balance Kazi Na Maisha Ya Ndoa, Malezi Ya
Watoto, Kutoa Msaada Wa Makazi, Kuwafundisha Wanaume Jinsi Ya Kushiriki Kwenye
Kazi Na Majukumu Ya Nyumbani, Kulea Watoto Na Kutoa Ushauri Wa Ajira Na Kazi.
Ukiachia Mbali Viwango
Vya Kuzaliana Kushuka Nchini Japan, Pia Viwango Vya Wanandoa Kupeana Talaka
Vimeongezeka Na Kuongeza Wasiwasi Kwa Serikali Ya Nchi Hiyo.
Majaribio Ya App Hiyo
Yamevutia Wengi Akiwemo Tajiri Wa Dunia Mmiliki Wa Mtandao Wa X Pamoja Na
Magari Ya Umeme Ya Tesla Elon Musk Ambaye Aliandika Yafuatayo Kwenye X “Nina
Furaha Serikali Ya Japan Inatambua Umuhimu Wa Jambo Hili, Endapo Hatua Kali
Hazitochukuliwa, Japan Pamoja Na Nchi Nyingine Nyingi Zitatoweka”