TAARIFA za uhakika kutoka
chanzo cha kuaminika zinasema wajumbe 3 wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC
kutoka upande wa Mwekezaji WAMEJIUZULU huku wengine 3 wakigoma kufanya hivyo
baada ya shinikizo kutoka kwa TAJIRI.
Wajumbe waliogoma KUTII
AMRI ya tajiri mpaka sasa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo SALIM ABDALLAH
MUHENE “Tryagain”, RASHIDI SHANGAZI ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo na HAMZA
JOHARI ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mamlaka za viwanja vya ndege Tanzania.
Mwekezaji anapaswa kuteua
wajumbe 7 kwa mujibu wa katiba lakini alikwisha teua 6 nafasi 1 ilikuwa
haijatumika mpaka sasa. Kawaida Bodi inakuwa na wajumbe 14 ambapo 7 wanapigiwa
kura na wanachama na 7 wanateuliwa na TAJIRI, kisha wajumbe hupiga kura
kuchagua Mwenyekiti wao ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi. Mpaka sasa Mwenyekiti
ni Salim Abdallah Muhene ‘Tryagain’.
Kikatiba wajumbe
wanahudumu kwa miaka 4 ndipo uchaguzi na uteuzi ili kuunda Bodi unafanyika
upya. Kitendo cha wajumbe ya Bodi wanaotokana na mwekezaji kujiuzulu kinatoa
picha ya kwamba yaliyokuwa yanasemwa ni kweli kwamba upande wa Mwekezaji UMESHINDWA
kuwajibika ipasavyo.
Stori zaidi zitaendelea
kaa chonjo saa mbaya……, tutawaletea mbivu na mbichi.
JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA HAPA KUJISAJIRI