MGOMBEA Wa Urais Kupitia
Cha Republican Donald Trump Amesema Ikiwa Atashinda Uchaguzi Wa Mwezi Novemba,
Huenda Akaziwekea Ushuru Nchi, Zinazoshindwa Kudhibiti Mmiminiko Wa Wahamiaji
Wasio Na Vibali Wanaoingia Marekani.
Trump Amesema Siku Ya Alhamisi
Kwamba Nchi Atakazoziwekea Ushuru Ni Pamoja Na China.
Trump Ametoa Matamshi
Hayo Akiwa Katika Jimbo La Arizona Alipokuwa Akijibu Maswali Ya Wakaazi Wa Eneo
Hilo, Ingawa Hakufafanua Ukubwa Wa Ushuru Atakaouanzisha.
Alipoulizwa Kuhusu Njia
Atakazotumia Kudhibiti Mmiminiko Huo Wa Wahamiaji Wanaoingia Kinyume Cha Sheria
Nchini Humo, Trump Alisema Tu Kwamba Marekani Ina Nguvu Kubwa Kiuchumi Na
Kuongeza Kuwa Ikiwa Nchi Kama China Haisaidii Kudhibiti Wahamiaji Wanaoingia Marekani,
Basi Atatumia Njia Kama Hiyo Ya Ushuru.
Usalama Wa Mpakani
Umekuwa Ajenda Muhimu Kwa Wamarekani Katika Uchaguzi Utakaofanyika Novemba 5,
Na Kuwakutanisha Trump Na Rais Joe Biden.